A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, September 13, 2020

RAIA WA KIGENI WADAKWA NA POLISI KWA WIZI KWA MTANDAO DAR



Dar es Salaam.
JESHI  la polisi  Kanda maalumu ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwakamata majambazi 9 wanaotapeli watu kwa njia ya mtandao miongoni mwao saba wakiwa ni raia wa Tanzania.
Kamanda Lazaro Mambosasa aliwaeleza waandishi wa habari kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako wa polisi .
Aliwataja watuhumiwa haoambao ni  kutoka mataifa mbalimbali ya kigeni waliokamatwa kwa tuhuma za kufanya uhalifu kwa njia mtandao (CYBER CRIME) na kuwa ni pamoja na Adewale Nuren Oyedes (34) Raia wa Nigeria ,Ibrahim Darbey (44) Raia wa Liberia Cream Milton Elias (38) Raia wa Liberia ,Basube Dominic (44), Raia wa DRC na Prince  Tito(46) raia wa Liberia .
Wengine ni  Sibongile Arhur  (44), Raia wa Afrika Kusini na Baljit Sigh (28), Raia wa India.
Kamanda   Mambosasa alisema kutokana uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo umewakamata watuhumiwa hao kwa mujibu wa sheria na ametoa onyo kwa wale wote wanaondelea kufanya vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwaomba wananchi kutoa taarifa wanapobaini kuwepo kwa matukio kama hayo
Katika hatua nyingine Kamanda Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kujifanya maofisa usalama wa Taifa, Polisi na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambao ni Patrick Tarimo (32) wa Mwenge anajitambulisha kama Afisa usalama wa Taifa. 
"Castory Wambura (57), mkazi wa Kibamba, anajitambulisha kama Ofisa wa Polisi na kwamba watuhumiwa wote wawili wamekuwa wakitapeli raia wema kwa kujifanya waajiriwa wa Idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi"
Mtuhumiwa Patrick Tarimo mnamo tarehe 10/08/2020 alijipatia kiasi cha Tsh 20,000,000/= kutoka kwa raia wa kigeni ambapo alimkamata na kujitambulisha kuwa yeye ni afisa usalama wa Taifa na kufanikiwa kujipatia kiasi hicho” alisema Mambosasa.
“Kwa upande wa mtuhumiwa Castory Wambura mnamo tarehe 21/08/2020 alitapeli kiasi cha Tsh 15,000,000/= kutoka kwa wafanyabiashara watano wa kariakoo, ambapo alijitambulisha kuwa yeye ofisa wa Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages