A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, August 17, 2020

WAFANYABIASHARA WAHIMIZWA KUJIUNGA MTANDAO WA WATEJA WAKUBWA WA BENKI YA NMB

 Benki ya NMB imewahimiza wafanyabiashara nchini kujiunga na Mtandao wa wateja wakubwa (NMB Business Executive Network) kujua na kunufaika na fursa za elimu juu ya mpangilio na uendeshaji biashara, kodi na taratibu za Serikali kuhusu biashara.


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akisalimiana na Afisa Mkuuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Severine Lalika.

Akizungumza jijini Mwanza juzi katika wa mkutano wa mtandao huo wa Kanda ya Ziwa, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB - Filbert Mponzi alisema wafanyabiashara wanaojiunga na mtandao huo pia hupata fursa kukutana na kujadiliana ana kwa ana na uongozi wa juu wa benki hiyo.

 “Kupitia vikao vya kila mwaka vya NMB Business Executive Network wafanyabishara hupata elimu kutoka kwa wataalam wa fani mbalimbali kuhusu namna bora ya kufanya biashara kirahisi, kwa tija na gharama nafuu kupitia teknolojia,” alisema Mponzi.

Sehemu ya wageni waalikwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages