A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, August 11, 2020

BENKI YA UBA YATOA DOLA MILIONI 200 KUSAIDIA SEKTA YA MAFUTA NIGERIA

 

Mwenyekiti Makampuni ya UBA, Tony O. Elumelu.
Lagos - Benki ya UBA imekuwa mwezeshaji mkuu (lead arranger) wa upatikanaji wa mkopo wa jumla ya Dola za Marekani bilioni 1.5 ili kufanikisha mradi wa uzalishaji wa mafuta unaoendeshwa na Shirika la Taifa la Petroli la Nigeria (National Petroleum Corporation - NNPC).

NNPC, kwa kupitia Kampuni ya Maendeleo ya Petroli ya Nigeria (Nigerian Petroleum Development Company - NPDC), inahitaji jumla ya Dola za Marekani bilioni 1.5 ili kuongeza uwezo wake wa uzalishaji mafuta.

Benki ya UBA itatoa Dola za Marekani milioni 200 ili kuwezesha kuongezeka kwa kiwango cha uwekezaji cha kampuni hiyo pamoja na kuboresha ukwasi wake katika uendeshaji.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages