Kadi hizo zinatumia teknolojia ya kisasa zaidi ya malipo duniani ambayo inamuwezesha mtumiaji kufanya malipo kwa haraka zaidi katika mashine za POS kwa kugusa bila kuingiza kadi ndani ya mashine ya malipo (POS)
Dar es Salaam. Agosti 5, 2020 - Katika kuongeza ubora wa huduma za kadi, BancABC leo imezindua kadi mpya za malipo maarufu kama ‘Gusa ulipe’ ili kuwawezesha wateja wake kufanya malipo kwa urahisi, haraka na usalama. Teknolojia hiyo ni ya kisasa zaidi katika kufanya malipo na ni salama na ya uhakika kwa watumiaji.
Teknolojia hii inaleta mageuzi makubwa kwenye huduma za malipo kwani kwa sasa wateja wataweza kufanya malipo kwa urahisi zaidi kwa kugusisha kadi kwenye mashine ya POS tofauti na ile ya awali ya kuchanja (swipe) au kuchomeka kadi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Meneja Mkuu wa kadi na teknolojia za kidijitali wa benki hiyo, Bwana Lameck Mushi alisema kadi hizo zitaleta urahisi wa malipo kwa kadi kwa wateja na kupelekea uharaka wakati wa kufanya miamala hivyo kuboresha huduma za malipo kwa njia ya kadi.
“Kadi hizi za VISA zinatumia mfumo unaokuwezesha kufanya malipo ya haraka mahala popote na inaondoa ulazima wa kutembea na pesa taslimu ili kulipia huduma mbalimbali. Teknolojia hii inaongeza ufanisi wa malipo kwa wateja wetu kwa sababu mchakato wake ni rahisi na salama zaidi,” alisema bwana Mushi.

No comments:
Post a Comment