A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, July 3, 2020

RAIS MAGUFULI ASHUSHA NEEMA JIMBO LA UKONGA, RC MAKONDA ATHIBITISHA KUPOKEA FEDHA ZA UJENZI WA BARABARA MPYA ZA LAMI ZENYE UREFU WA KM 29.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Jimbo la Ukonga Kivule wakati wa  Mwendelezo wa Ziara ya kukabidhi Miradi kwa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Ukonga ambapo ameeleza mpango mzima wa ujenzi wa barabara miongoni mwa Barabara za Km 12 za kutoka Kwa Mpalange kwenda Kilungule,Mwanagati,Kitunda na kuishia Banana zitajengwa kwa kiwango cha lami.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Jimbo la Ukonga Chanika wakati wa  Mwendelezo wa Ziara ya kukabidhi Miradi kwa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Ukonga ambapo ameeleza mpango mzima wa ujenzi wa barabara miongoni mwa Barabara za Km 12 za kutoka Kwa Mpalange kwenda Kilungule,Mwanagati,Kitunda na kuishia Banana zitajengwa kwa kiwango cha lami. Picha zote na Brian Peter

Kufuatia kilio cha Muda mrefu cha Wananchi wa Jimbo la Ukonga na juu ya Ubovu wa Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Rais Dkt. John Magufuli ameridhia kutoa fedha za Ujenzi wa Barabara Mpya jimboni humo kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Km 29 Chini ya Mradi wa DMDP kwa fedha kutoka Bank ya Dunia.

RC Makonda amesema hayo wakati wa Mwendelezo wa Ziara ya kukabidhi Miradi kwa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Ukonga ambapo ameeleza miongoni mwa Barabara hizo ni Km 12 za kutoka Kwa Mpalange kwenda Kilungule,Mwanagati,Kitunda na kuishia Banana.

Aidha RC Makonda amesema barabara nyingine zinazojengwa ni Km 16.6 kuanzia Pungu Majoe kupitia kwa Mngondole, Kivule hospital na kuishia Kitunda pamoja na km 5 inayoanzia Chanika kupitia Msumbiji kuelekea Homboza.

Pamoja na hayo RC Makonda amemuelekeza Mkandarasi wa mradi usambazaji umeme wa REA kata 8 na mitaa 25 ya Zingiziwa kuhakikisha ifikapo Agost 31 mitaa yote iwe imeunganishwa na umeme kwa gharama ya Tsh 27,000 na sio 320,000 iliyopangwa na TANESCO.

Katika ziara hiyo RC Makonda amekabidhi kwa Chama cha mapinduzi miradi mbalimbali ikiwemo Machinjio ya Vingunguti, Hospital ya Wilaya ya Kivule A na B, Mitambo ya Umeme Kinyerezi one na Two, Mtambo wa Gas wa TPDC na Mradi wa kusambaza umeme Zingiziwa.

Miradi mingine ni Ujenzi wa Soko la Kisutu, Jengo la Abiria la Terminal Three, Ujenzi wa Daraja la Ulongoni B, Ujenzi wa Barabara ya kuanzia Banana, Kitunda na Kivule zenye urefu wa Km 3.2.

MATUKIO KATIKA PICHA





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages