MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu raia wawili wa China na Mtanzania mmoja kutumikia kifungo cha jumla ya miaka 30 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya makosa matano kati ya sita likiwemo la kukwepa kodi na kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hasara ya Sh. Bilioni 1.776/=
Aidha mahakama imeamuru washtakiwa hao wakimaliza kutumikia kifungo walipe fidia ya kiasi hicho cha fedha walichosababisha hasara.
Washtakiwa waliohukumiwa leo ambao ni raia wa China ni wafanyabiashara Gu Kai (49) mkazi wa Kariakoo na Jason Wei (30) anayeishi Tabata Matumbi pamoja na Jovin James (28) mtanzania anayeishi Tabata.
Aidha mahakama imemuachia huru Leornad Assey (26), baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.
Hukumu hiyo imesomwa na hakimu Mkazi Mkuu wa Huruma Shahidi ambaye amesema, upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake tisa waliofika mahakamani kutoa ushahidi, wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shtaka kuwa washtakiwa hao watatu ametenda makosa hayo matano na amewaachia huru katika kosa moja la kula njama.
Akifafanua adhabu hiyo Hakimu Shaidi amedai, Katika shtaka la kughushi washtakiwa watatumikia kifungo cha miaka saba na katika kosa la kutoa nyaraka za uongo wamehukumiwa miaka saba huku shtaka la kujipatia usajili kwa udanganyifu miaka miwili kusababisha hasara miaka sana pamoja na kosa la kukwepa kodi.
Hata hivyo adhabu zote nitaenda pamoja hivyo, watakaa gerezani kwa miaka saba.
Pia, wakati hukumu hiyo inasomwa mshtakiwa Wei hakuwepo mahakamani baada ya kuruka dhamana na mahakama imeamuru atafutwe ili ianze kutumikia kifungo chake.
Aidha kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, Hakimu Shahidi aliuliza kama upande wa mashtaka walikuwa na lolote la kusema ndipo wakili Anna Chimpaye akasema hawana kumbukumbu za zamani za washtakiwa lakini wameiomba mahakama kutoa adhabu kali kwani kosa walilofanya limeitia hasara serikali.
Katila kesi ya msingi washtakiwa wote wanadaiwa, mwaka 2014 jijini Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa ambapo wanadaiwa Oktoba 21, 2014 Dar es Salaam walighushi fomu ya taarifa za mteja wakionesha kwamba kampuni ya Calcare international company ltd imeomba mashine ya EFD kwa Compulynx Tanzania Ltd wakati siyo kweli.
Katika shtaka la tatu imedaiwa kuwa siku na mahali hapo mshtakiwa Jovina na Gu Kai waliwasilisha kwa Compulynx T Ltd fomu ya taarifa ya mteja wakidai kwamba kampuni ya Calcare iliomba mashine ya EFD huku wakijua kuwa siyo kweli.
Katika shtaka la nne imedaiwa, siku na mahali hapo washtakiwa kwa nia ya kudanganya walijipatia usajili wa EFD mashine kutoka TRA kwa kujidai kwamba mashine hiyo ingetumiwa na Calcare huku wakijua kuwa siyo kweli.
Imeendelea kudaiwa kuwa, kati ya Oktoba 21 2014 na Machi 30 2016 jijini Dar es Salaam washtakiwa Leornad na Jason wakiwa watu wanaojihusisha na uendeshaji wa shughuli za kampuni za Tifo Global Mart (Tanzania) na Lotay Steel ( Tanzania) Ltd kwa nia ya kudaganya walitumia EFD mashine iliyosajiliwa na Calcare na kukwepa kodi ya sh 1,776,693,465/=
Katika shtaka la mwisho inadaiwa kuwa, katika kipindi hicho hicho washtakiwa wote kupitia vitendo vyao waliisababishia TCRA hasara ya Sh. 1,776,693,465/= kwa kusajili EFD mashine na baadae kuitumia kutoa risiti feki kufuatia mauzo yaliyofanywa na kampuni ya Tifo na Lotay.
Washtakiwa wakipanda kwenye gari la magereza jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuhukumiwa.
No comments:
Post a Comment