A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, July 28, 2020

Kocha Mtibwa: Nipo Tayari Kutupiwa Virago

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema kuwa yupo tayari kuwajibishwa na uongozi wa klabu hiyo kufuatia mwenendo mbaya katika ligi kuu msimu huu.

Katwila alisema anastahili hata kujiuzulu au kufutwa kazi kama viongozi watafikia uamuzi huo, ingawa mara zote dhamira yake ilikuwa ni kuiongoza Mtibwa Sugar katika kuyafikia malengo ya kufanya vizuri katika kila msimu.

Huu ni msimu mbaya zaidi kwa Mtibwa Sugar kuwahi kutokea tangu timu hiyo ilipopanda kucheza ligi kuu kwa kuwa ipo miongoni mwa timu saba ambazo hazikuwa na uhakika wa kusalia katika ligi kuelekea michezo ya mwisho ya ligi jana Jumapili. Na ilitakiwa ihakikishe inashinda katika mchezo wa mwisho dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Katwila alisema: “Nipo tayari ‘ku-resign’ (kujiuzulu) kwa sababu ya matokeo mabaya, kama kocha ninatakiwa kuiongoza timu kushinda. Malengo yangu na ya kocha yeyote kwenye timu ni kuhakikisha anaipa mafanikio timu katika kila msimu, lakini mambo yamekuwa tofauti kwangu kwa msimu huu, kwa hiyo nipo tayari kufutwa kazi kama viongozi wataamua hivyo.”

Mtibwa walikuwa katika nafasi ya 15 kabla ya mchezo wa juzi wakiwa na pointi zao 42 na walicheza na Ruvu ambayo yenyewe kimahesabu angalau ilionekana kuwa bado ipo salama kwani ilikuwa nafasi ya 11 na pointi 47 na hata kama walipoteza waliweza kuwa na nafasi kwa msimu ujao kutokana na alama za timu zilizofuatia chini yake kama KMC, Lipuli na Mwadui.

Huu ni msimu wa tatu wa Katwila akiinoa Mtibwa Sugar akiwa amefanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi mara moja.
ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages