A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, July 28, 2020

Dewji Atuma Ombi Kwa JPM Kumuenzi Mkapa

BILIONIEA mwekezaji kwenye Klabu ya Simba Mohamed Dewji ‘MO’ ametuma maombi kwa Rais Dk John Magufuli kubadili jina la Uwanja wa Taifa na kuwa Uwanja wa Benjamin William Mkapa.

Mfanyabiashara huyo amesema itakuwa ni heshima kubwa kama uwanja wa Taifa utaitwa Uwanja wa Benjamin William Mkapa kutokana na mchango mkubwa wa mzee Mkapa kwenye michezo.

“Tunamuomba Rais Dk John Pombe Magufuli aridhie kubadili jina la uwanja huo kwa heshima ya Hayati Mkapa ili tuendelee kumkumbuka kwa mchango wake mkubwa na hasa kwa vizazi vijavyo,” ameeleza Dewji kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa twitter.

Ameeleza kuwa uwanja huo kwa namna mmoja au nyingine umesaidia kuendeleza mpira wa miguu na michezo mingine nchini Tanzania.

“Uzuri na ukubwa wa soka letu umedhihirishwa kwa sababu ya uwanja wetu huo ambao unashika nafasi ya 11 kwa ukubwa Afrika…

“Uwanja huo wa kisasa pia umeongeza uzalendo mkubwa kwa kuwezesha maelfu ya mashabiki kuwa sehemu ya michezo yote mikubwa, pia umeongezea mapato kwa klabu zote na kutuletea heshima kubwa nchini na mifano ipo dhahiri,” alieleza Dewji.

Alisema kutokana na uzuri wa uwanja huo, klabu zote za nje ambao huja kucheza katika uwanja huo zimekuwa zikitoa sifa kama vile timu za mataifa makubwa kama Brazil zimecheza kwenye uwanja huo na kumwaga sifa mbalimbali.

Kadhalika nje ya michezo, Dewji alisema mashindano ya usomaji wa Quran aliona mkusanyiko mkubwa zaidi kwenye mashindano makubwa ya kusoma Quran barani Afrika, hii nayo ilikuwa ni rekodi nzuri kwetu Watanzania ndani ya uwanja huu.

“Tumeshuhudia matamasha mbalimbali makubwa kama matamasha ya Pasaka na Krsimasi yakifanyika hapo na lengo la yote hayo ni kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania,” alisema.

Ujenzi wa Uwanja wa Taifa wa jijini Dar es Salaam uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ulianzishwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa na unatajwa kuwa miongoni mwa viwanja bora katika bara la Afrika kwa sasa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages