A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, July 17, 2020

BENKI YA NMB YASHINDA TUZO YA KIMATAIFA YA BENKI BORA TANZANIA MARA NANE MFULULIZO

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin P. Mhede (katikati) akikabidhiwa Tuzo ya Benki Bora na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto). Akishuhudia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi (kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk.Edwin P. Mhede (katikati), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi (kulis) wakiifurahia Tuzo walioipokea kwa kuwa Benki Bora Tanzania.
Benki ya NMB imekuwa benki bora nchini Tanzania kwa mara ya nane mfululizo baada ya kuzibwaga benki zingine 40 nchini.

Tuzo hiyo imetolewa na Euromoney, ambalo ni jarida la kimataifa la masuala ya kifedha linaloongoza duniani lenye makao makuu yake jijini London, Uingereza.

Tuzo hii inaonesha kuwa Benki ya NMB ni zaidi ya taasisi inayotoa huduma za kifedha na kuwa kichocheo muhimu cha mabadiliko ya kiuchumi kupitia utoaji huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali.

Akiongea wakati wa kukabidhiwa tuzo hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NMB – Dk. Edwin Mhede alisema baada ya Tanzania kufikia uchumi wa kati, Benki ya NMB inaahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kuchangia zaidi katika ukuaji wa uchumi kwenda katika hatua ya juu zaidi.


Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB - Ruth Zaipuna alisema: “Leo hii tunajulikana kama benki imara zaidi, yenye huduma za ubunifu wa kiteknolojia. Tumedhamiria kuwa zaidi ya taasisi ya huduma ya fedha kwa kuendelea kuchochea mabadiliko ya kiuchumi katika nchi yetu na kuboresha maisha ya Watanzania wenzetu kwa kutoa huduma zinazowafaa na kukidhi mahitaji na mipango yao.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages