Na Woinde Shizza , Michuzi Tv Arusha
Benki ya CRDB imezindua rasmi mfumo mpya wa kidijitali "QR code"kwa kanda ya kaskazini ambao unamuwezesha mteja wa benki hiyo kutoa maoni, mapendekezo na mrejesho ambapo mteja atatumia simu janja kuweka maoni kwenye sanduku la maoni tofauti na ilivyozoeleka.
Akizungumza jijini Arusha mara baada ya kuzindua mfumo huo meneja wa bank hiyo kanda ya kaskazini Chiku Issa amesema CRDB inakuwa ya kwanza kuzindua mfumo huu ambao utawawezesha wateja kutoa maaoni ya huduma au malalamiko moja kwa moja ambayo yatapokelewa na kujibiwa bila kusubiri.
Uzinduzi huo ambao tayari umefanyika katika mikoa ya Dar es salaam na Mwanza kwa mkoa wa Arusha umezinduliwa katika tawi la Arusha ambapo wateja wa benki hiyo wamehudhuria na kushuhudia namna ambavyo mfumo huo unavyofanya kazi kwa ufanisi.
“Hii ni huduma ambayo itahakikisha wateja wetu wanakuwa karibu Zaidi na benki na kupata huduma nyingi Zaidi na kutoa maoni yao yatakayoweza kusaidia benki yetu iweze kuendelea vizuri”alisema Chiku.
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja bank ya CRDB Yolanda Urio amesema mfumo huo ni rahisi, salama na haraka kwa kuwa mteja hupata mrejesho kwani mteja anachotakiwa kufanya ni kupakua application tu.
"Mfumo huu umeunganishwa na mifumo mingine na unampa fursa mteja wa CRDB kupata huduma mbalimbali " alisema Urio
Mmoja wa wateja wa benki ya CRDB Charles Hotay amesema huduma hiyo ni mkombozi kwao kwa sababu kuna nyakati mteja anahitaji utatuzi wa changamoto fulani kwa haraka lakini walikuwa wanalazimika kwenda bank kuuliza au kujaza fomu na kuweka kwenye kisanduku ambapo hatukujibiwi kwa wakati.
Naye Dina Patrick mteja aliyehudhuria kwenye uzinduzi huo amesema mbali na kusaiidia wateja wa CRDB mfumo huu unamanufaa Zaidi kwa kuwa utasaidia wanafunzi ambao mara nyingi hutumia mitandao kulipia huduma mbalimbali na watakapo kwama ni rahisi kupata utatuzi.
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja bank ya CRDB Yolanda Urio na viongozi mbalimbali wa CRDB wakikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa mfumo mpya wa QR CODE kwa kanda ya kaskaziniunaomuwezesha mteja kutoa maoni ya huduma au malalamiko moja kwa moja ambayo yatapokelewa na kujibiwa bila kusubiri
Meneja wa benki ya CRDB kanda ya kaskazini Chiku Issa akikata keki katika uzinduzi wa mfumo mpya wa kidigital "QR CODE "katika hafla iliyofanyika kwenye tawi la CRDB Arusha.(picha na Woinde Shizza).
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja bank ya CRDB Yolanda Urio akimuelekeza mteja wa benki hiyo Bw.Charles Hotay namna ya kutumia mfumo mpya wa kutoa malalamiko kwa benk kwa haraka wa QR CODE(picha na Woinde Shizza )
No comments:
Post a Comment