A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, June 10, 2020

Mwanzo Mgumu Kwedikwazu walilia usafiri


Na Omary Mngindo, Tanga


WAJASIRIAMALI wa Kikundi cha Mwanzo Mgumu, kilichopo Kijiji cha Kwedikwazu Kata ya Kabuku wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga, wanahitaji usafiri utaowarahisishia kazi zao za ubebaji wa mawe.

Wakizungumza na Waandishi wa habari katika eneo wanalofanya shughuli zao za kubangua mawe, Wajasiriamali hao walisema kuwa wananufaika na machimbo ya mawe yanayotumika kutengenea Marumaru na Jipsam katika majengo mbalimbali.

Katibu wa kikundi hicho Saumu Kisaka alisema kuwa wananunua mawe kutoka katika Makampuni yanayochimba mawe Kijijini hapo, wananunua plastiki moja shilingi elfu 2,000 wanayabangua kisha wanauza kwa shilingi 3,000, hivyo wanapata pesa za kujikimu na familia zao.

Asia Omary Mjumbe alisema kuwa kikindi chao kilikopa shilingi milioni 5 kutoka Halmashauri ya Handeni, ambazo wanataraji kuumaliza wakati wowote, na kwamba wanataraji kukopa pesa zaidi kwa ajili ya kukiendeleza biashara yao.

"Tunakutana kila wiki ambapo kila mwanachama anachangia shilingi 5,000 mpaka sasa tuna kiasi cha shilingi milioni 2 benki, lakini moja ya changamoto nyingine tunayokabiliana nayo ni ubanguaji wa mawe haya kwa mikono," alisema.

Kibibi alisema kuwa wakimaliza mkopo wa Halmashauri wanataraji kuomba mkopo wa milioni kumi, lakini kiu yao ni kumiliki gari ndogo watahoitumia kubeba mawe kutoka katika machimbo yaliyopo kijijini hapo.

"Tutaomba uahauri kutoka kwa viongozi wetu, hususani diwani na wataalamu wemgine tuone ni namna gani anavyoweza kutushauri katika hili kwani lengo letu kubwa ni kumiliki chombo cha moto kotachotusaidia kubeba mawe," alisema Kibibi.

Nae Mwenyekiti wa Mwanzo Mgumu Zaina Mwelugala aliishukuru Serikali chini ya rais Dkt. John Magufuli kwa juhudi kuhimiza viwanda, kwani nao wananufaika kupitia wawekezaji waliopo ikiwemo wao kununua mawe, kuyagonga kisha kuuza kokoto.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages