A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, June 10, 2020

Iran yazitaka Urusi na China kuzuwia juhudi za marekani kurefusha vikwazo

Iran imetoa wito leo kwa Urusi na China kupinga juhudi za Marekani kurefusha vikwazo vya silaha viliyowekwa na Umoja wa mataifa ambapo muda huo utafikia mwisho mwezi Oktoba chini ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani mwaka 2015.

Utawala wa rais Donald Trump wa Marekani umekuwa ukichukua msimamo mkali kwa Umoja wa Mataifa kurefusha na kuimarisha marufuku dhidi ya Iran, ikionya kuwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo kutaifanya Iran kupata silaha ambazo zinaweza kuchochea mizozo katika mashariki ya kati.

Iran na hasimu wake Saudi Arabia, mshirika wa karibu wa Marekani zimehusika katika vita nje ya nchi zao pamoja na misuguano ya kisiasa katika kanda hiyo kwa miongo kadhaa, kuanzia Iraq na Syria hadi Bahrain na Yemen.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages