A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, May 19, 2020

Waziri Biteko: Sekta Ya Madini Inaongoza Kwa Ukuaji Nchini,Makusanyo Yamepaa Kutoka Bilioni 39/- Hadi Bilioni 58/- Kwa Mwezi Aprili

B32A9791
Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wajumbe wa warsha iliyoandaliwa kwa lengo la kuandaa kitabu cha viashiria hatarishi (Risk Registry) vya Wizara ya Madini iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Augustine Ollal. (Picha na Wizara ya Madini).
B32A9797
Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wajumbe wa warsha iliyoandaliwa kwa lengo la kuandaa kitabu cha viashiria hatarishi vya Wizara ya Madini (hawapo pichani) iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma Mei 18, 2020.
B32A9805
B32A9807
 Wajumbe wa warsha iliyoandaliwa kwa lengo la kuandaa kitabu cha viashiria hatarishi vya Wizara ya Madini iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma Mei 18, 2020 wakimfuatilia Waziri wa Madini, Doto Biteko. Mbele ni Mwezeshaji Dkt.Ernest Mwasalwiba. (Picha na Wizara ya Madini).

B32A9810
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) na Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila wakiteta jambo wakati wa warsha iliyoandaliwa kwa lengo la kuandaa kitabu cha viashiria hatarishi vya wizara ya madini iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma Mei 18, 2020. (Picha na Wizara ya Madini).
B32A9823
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Madini, Augustine Ollal akiwakaribisha viongozi wakuu wa wizara kwenye ufunguzi wa warsha ya kuandaa kitabu cha viashiria hatarishi vya wizara. Katikati ni Waziri wa Madini, Doto Biteko na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila. (Picha na Wizara ya Madini).


B32A9824
Mwezeshaji Dkt. Ernest Mwasalwiba wa warsha iliyoandaliwa kwa lengo la kuandaa kitabu cha viashiria hatarishi vya Wizara ya Madini iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma Mei 18, 2020 akiendelea na kutoa mafunzo kwa washiriki. (Picha na Wizara ya Madini).
B32A9830
Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa (kushoto) akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini, Issa Nchasi na wajumbe wengine wakifuatilia mafunzo juu ya uandaaji wa daftari la viashiria hatarishi. (Picha na Wizara ya Madini).
B32A9831
Mwezeshaji Dkt. Ernest Mwasalwiba wa warsha iliyoandaliwa kwa lengo la kuandaa kitabu cha viashiria hatarishi vya Wizara ya Madini iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma Mei 18, 2020 akiendelea na kutoa mafunzo kwa washiriki (hawapo pichani). (Picha na Wizara ya Madini).

Nuru Mwasampeta na Tito Mselemu,WM- Dodoma

WAZIRI wa Madini, Doto Biteko amesema ukuaji na mchango wa Sekta ya Madini kwenye pato la taifa unakua kwa kasi na kuwa mwaka 2019 mchango huo umeongezeka na kufikia asilimia 17.7 kutoka ukuaji wa asilimia 1.5 kwa mwaka 2018.

Amesema, kwa ukuaji huo sekta ya madini imeongoza sekta zote kwa ukuaji ikifuatiwa na sekta ya ujenzi ikiwa na ukuaji wa asilimia 14.1.

Ameongeza kuwa, wizara yake imekuwa ikikusanya kiasi cha wastani wa shilingi bilioni 39 kwa mwezi ,lakini kwa mwezi Aprili makusanyo hayo yamepaa na kufikia kiasi cha shilingi bilioni 58 jambo ambalo linaonesha mafanikio makubwa ya kisekta.

Hata hivyo, Waziri Biteko ametaka ukuaji huo wa Sekta ya Madini usaidie katika kukuza sekta nyingine za kiuchumi na hapo ndipo manufaa ya sekta ya madini yatakuwa na manufaa zaidi.

Waziri Biteko amebainisha hayo alipokuwa akifungua warsha ya maandalizi ya kitabu cha viashiria hatarishi (Risk register) cha wizara inayofanyika kwa siku tano katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI) na baadaye kuja na kitabu hicho kama matokeo ya warsha hiyo.

Biteko ameongeza kuwa, wizara inapoendelea kutekeleza majukumu yake, yumkini kuna viashiria hatarishi ambavyo endapo havitadhibitiwa vitakwamisha juhudi za wizara kufikia malengo, hivyo wizara imeamua kuandaa kitabu kitakachosaidia kubaini viashiria hivyo na kuvifanyia kazi ili kuyafikia malengo iliyojiwekea.

Akizungumza na washiriki wa warsha hiyo, Biteko amewataka wajumbe kubaini viashiria hatarishi vinavyoikabili wizara, kubuni mikakati madhubuti ya kudhibiti viashiria hivyo na kuandaa daftari la viashiria hatarishi la wizara kwa muda wa siku tano watakazokuwepo katika warsha hiyo.

Amesema, kwa kufanya hivyo, uhakika wa wizara pamoja na wadau wake wa malengo mkakati ya wizara kufikiwa utakuwa mkubwa kwani viashiria hatarishi vitakuwa vimepangiwa mikakati ya kuidhibiti kabla ya kutokea na kukwamisha juhudi za wizara.

Biteko amesema, maandalizi ya kitabu cha viashiria hatarishi ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa katika Waraka wa Hazina namba 12 wa mwaka 2013 ukielekeza taasisi zote za umma zikiwemo wizara kuwa na mfumo thabiti wa kudhibiti viashiria hatarishi (Risk Management) na kuandaa daftari la viashiria hatarishi (Risk register)

Ameendelea kusema suala la udhibiti na usimamizi wa viashiria hatarishi ilianzishwa mwaka 2010 kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho kati sura 348 ya Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2001.

Waziri Biteko amesema usimamizi wa viashiria hatarishi kwenye taasisi za umma ni takwa la kisheria ambapo chimbuko lake ni marekebisho katika sura ya 348 ya Sheria ya Fedha za umma ya mwaka 2001 yaliyofanyika mwaka 2010 na hivyo kuanzishwa kwa Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali ambapo moja ya majukumu yake ni kusimamia mifumo ya udhibiti wa viashiria hatarishi vya malengo katika taasisi za umma.

Aidha, Waziri Biteko amewataka watendaji wa wizara kuendelea kuwakumbusha wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuendelea kufuata sheria na taratibu zinazosimamia Sekta ya Madini ili iendelee kuzalisha kwa faida.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amewataka washiriki wote kufuatilia kwa umakini mafunzo hayo ili kuvitambua viatarishi na kuviepuka kabla havijawa tatizo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages