A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, May 19, 2020

BALOZI WA KENYA NCHINI TANZANIA AFUNGUKA


Balozi wa Kenya nchini Tanzaniai Danny Kazungu leo tarehe 19 Mei amezungumza na waandishi wa habari kufuatia kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na kufungwa kwa mpaka kati ya Kenya na Tanzania.

Akizungumza katika ubalozi wa Kenya uliopo Jijini Dar es Salaam Balozi huyo Amesema ametumwa na Rais Kenyatta kuzungumza na Watanzania kupitia vyombo vya habari na kusema kuwa nchi ya Kenya na Tanzania haziishii tu kwenye ujirani Bali ni ndugu pia.

“Rais Kenyatta amenituma hapa, anasema Kenya haiiangalii Tanzania kama jirani bali kama Ndugu, sisi sio maadui, adui yetu ni corona, ndio maana alikuwa Rais wa kwanza kuingia Chato kumsalimia JPM, akachukua dhahabu akasema mpelekeeni Maguful" Amesema Balozi Kazingu.

‘Bila hii Corona April 26 mwaka huu Kenyatta alipanga aje asherehekee na Watanzania Muungano, alipanga awe na ziara ya muda mrefu hapa TZ kuliko Rais yeyote, uamuzi ambao Kenya imechukua kuhusu safari za mipakani sio kwasababu ya Tanzania bali adui yetu ni kirusi” Balozi Kazungu

Aidha alisisiza kuwa hakuna Mkenya anaemuombea mabaya Mtanzania na badala yake wanawaombea Watanzania wote kwa ujumla ili waweze kulimaliza janga hili la Corona hivyo Watu wasikubali kukorogwa na Kirusi na kuharibu undugu uliopo.

"Hakuna Mkenya anayemuombea mabaya Mtanzania, Wakenya tunawaombea Watanzania mpigane na janga hili, na sisi pia mtuombee, tusianze kukorogwa na kirusi hiki, tusianze kugongana kisa corona, Watu watulie, Viongozi wetu watakutana na tutalimaliza” - Balozi Kazungu

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages