A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, March 24, 2020

RC MAKONDA: "DAR ES SALAAM TUNAANZA RASMI ZOEZI LA KUPULIZA DAWA YA KUUA WADUDU NA KUENEA KWA VIRUSI VYA CORONA KESHO"

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akizungumza na wananchi pamoja na wafanya biashara wa Stendi Kuu ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani ‘Ubungo Bus Terminal’, wakati alipotembelea kituo hicho kwa ziara maalum ya kukagua utekelezwaji wa agizo la Serikali juu ya kujikinga na gonjwa hatari la Corona (COVID 19) ambalo limekuwa tishio duniani kote, ziara hiyo imefanyika leo jijini huko. (Picha na Brian Peter)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda, akizungumza na wananchi pamoja na wafanya biashara wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jilius Nyerere, wakati alipotembelea Viwanjani hapo kwa ziara maalum ya kukagua utekelezwaji wa agizo la Serikali juu ya wananchi kujikinga na gonjwa hatari la Corona (COVID 19) ambalo limekuwa tishio duniani kote, ziara hiyo imefanyika leo jijini huko. (Picha na Brian Peter)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (mwenye shati jeupe), akimsikiliza Meneja wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Mahela Chilosa Nkhana wakati alipotembelea kituo hicho kwa ziara maalum ya kukagua utekelezwaji wa agizo la Serikali juu ya kujikinga na gonjwa hatari la Corona (COVID 19) ambalo limekuwa tishio duniani kote, ziara hiyo imefanyika leo jijini huko. (Picha na Brian Peter)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda, akipata maelezo kutoka kwa watumiaji wa ‘Ubungo Bus Terminal’
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda, akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Polisi upande wa Bandari alipotembelea nakukagua usalama katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda, akitoa elimu kuhusu ugonjwa wa Corona na jinsi ya kujikinga kwa abiria waliokuwa wakisafiri kutoka stendi ya mabasi Ubungo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda, akipatapa maelekezo kutoka kwa baadhi ya uongozi wa Kiwanja cha ndege Terminal 3 wakati wa ziara maalum ya kukagua utekelezwaji wa agizo la Serikali juu ya kujikinga na gonjwa hatari la Corona (COVID 19) ambalo limekuwa tishio duniani kote, ziara hiyo imefanyika leo jijini huko. (Picha na Brian Peter)

Moja ya abiria wa basi la Tashriff linalofanya safari zake Tanga-Dar na mikoa mingine, akinawa mikono kabla ya kupanda kwenye basi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amesema mkoa huo utaanza rasmi kesho zoezi la kupuliza dawa ya kuua vijidudu na kudhibiti kuenea kwa Virusi vya Corona katika maeneo mbalimbali ya Jiji hilo ambapo amewataka wananchi wasiwe na hofu pindi wanapoona magari yanapita mitaani kupuliza dawa.

RC Makonda amesema kwa kufanya hivyo  itasaidia pia kuua Vimelea na Wadudu kama Mbu wanaoenzeza ugonjwa wa Malaria, homa ya dengu na magonjwa mengineyo na kufanya jiji hilo kuwa katika hali nzuri ya kuwakinga wananchi wake.

Mhe. Makonda amesema hayo wakati alipofanya Ziara kwenye Maeneo yanayopokea Wasafiri kutoka nje ya Nchi ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo na Bandarini kwa lengo la kukagua namna walivyojipanga kudhibiti kuenea kwa Virusi Vya Corona ikiwemo namna ya wanavyowahudumia Wasafiri kuanzia Vipimo.

Aidha RC Makonda ameonyesha kuridhishwa na namna taasisi hizo zimejidhatiti kuwahudumia Wasafiri kutoka Ndani na Nje ya Nchi kuanzia unawaji wa mikono na kuchukuliwa vipimo vya joto ambapo amewahimiza kuhakikisha kila mgeni anaeingia Nchini anachukuliwa na kuwekwa kwenye uangalizi kwa siku 14.

Pamoja na hayo RC Makonda amewaelekeza wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi kuhakikisha wanaweka Vyombo vya kunawa mikono mwanzo wa safari na mwisho wa safari ikiwa ni pamoja na kufanya usafi wa gari kila Mara.

Hata hivyo RC Makonda amewataka Wananchi kuendelea kujikinga na Virusi vya Corona kwa kunawa nikono na maji yenye Dawa, kuepuka kujazana kwenye vyombo vya usafiri, kuepuka safari zisizo na ulazima pamoja na kuepuka Mikusanyiko.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages