A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, March 24, 2020

BENKI YA NMB YAKABIDHI MSAADA WA VITI, MEZA NA MADAWATI VYA THAMANI YA SH. 15M/- KWA AJILI YA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI UBUNGO

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (kushoto) akimkabidhi msaada wa madawati, viti na meza 150 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori (kulia) katika Shule ya Sekondari Kibamba. Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 15 vimetolewa na Benki ya NMB kuzisaidia Shule tatu za Manispaa ya Ubungo ambazo ni Kibamba, Kinzudi Sekondari pamoja na Shule ya Msingi Makuburi Jeshini zote za jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori (kulia mwenye suti) pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (wa pili kushoto) wakikata utepe kuzinduwa madawati, viti na meza 150 katika Shule ya Sekondari Kibamba, vilivyotolewa na Benki ya NMB kuzisaidia Shule tatu za Manispaa ya Ubungo ambazo ni Kibamba na Kinzudi Sekondari na Shule ya Msingi Makuburi Jeshini kutatua changamoto za madawati leo katika Manispaa ya Ubungo.

Benki ya NMB, imekabidhi msaada wa viti, meza na madawati vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 15 kwa ajili ya Shule za Sekondari Kibamba na Kinzudi na Shule ya Msingi Makuburi Jeshini, zilizoko wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam.

Hafla ya kukabidhi msaada huo ilifanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kibamba, ambako Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd alimkabidhi msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori (aliyekuwa mgeni rasmi).

Alisema Kibamba Sekondari yenye wanafunzi 1,365, ilikuwa na changamoto ya uhaba wa viti na meza na kwamba msaada wa NMB unaenda kupunguza kwa kiasi kikubwa adha ya wanafunzi kusoma katika mazingira yasiyo rafiki.

Naye Ofisa Elimu (Sekondari) Wilaya ya Ubungo, Hilda Shalanda, alisema kinachofanywa na benki ya NMB katika wilaya yake kwenye sekta ya elimu, ni kitu cha kupongezwa na kinachopaswa kuungwa mkono na wadau wengine kwa kuzifikia shule mbalimbali zenye uhitaji.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages