A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 23, 2020

RC MAKONDA AMTAKA MKANDARASI WA UJENZI WA BARABARA YA MABASI YA MWENDOKASI MBAGALA KUONGEZA SPEED



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda (kulia) akikagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, inayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200 leo Machi 23, 2020 ambapo amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuongeza kasi ili mradi ukamilike na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa Mbagala.

Mafundi wakiendi kazi ya ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.


Muonekano wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akikagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, inayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200 leo Machi 23, 2020 ambapo amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuongeza kasi ili mradi ukamilike na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa Mbagala.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, inayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200 leo Machi 23, 2020 ambapo amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuongeza kasi ili mradi ukamilike na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa Mbagala.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea na kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala inayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200 ambapo amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuongeza kasi ili mradi ukamilike na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa Mbagala.

RC Makonda amesema kwa muda mrefu wakazi wa Mbagala walikuwa wakipata changamoto ya usafiri ikiwemo foleni na wakati mwingine wananchi kuibiwa simu na mikoba wakiwa wanagombania usafiri lakini kukamilika kwa mradi huo itakuwa mwarobaini wa kero zote zilizokuwa zikiwasumbua.

Aidha RC Makonda amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutafanya Barabara ya Kilwa kuwa na Njia sita, Madaraja Mawili Makubwa na Flyover jambo litakalosaidia kurahisisha shughuli za usafiri.

Aidha RC Makonda amezungumzia changamoto ya Mafuriko Mto Msimbazi kujaa eneo la Jangwani na kusababisha kusimama kwa shughuli za usafiri ambapo amesema Serikali ipo katika hatua ya kuanza kwa maboresho ya eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuinua Daraja na kufanya mto msimbazi kuwa sehemu ya utalii wa Boti ambapo ujenzi unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi Bilioni 200.

Kuhusu Ugonjwa wa Corona, RC Makonda amesema tayari amewaelekeza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanatenga maeneo maalumu ya kuwahifadhi watu wote wanaotoka nje ya Nchi (karantini) ili wakae chini ya uangalizi kwa muda wa siku 14 huku akiwahimiza wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari dhidi ya Virusi hivyo vya Corona.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages