A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, October 1, 2019

BENKI YA NMB YAAHIDI MAKUBWA KIKAO KAZI CHA MAOFISA WA POLISI

Kutoka kushoto: Kamishna wa Police, Operesheni na Mafunzo, Liberatus Sabas, Kamishna Msaidizi Mwandamizi: Mipango na Bajeti, Yustus Kamugisha, Kamishna wa Polisi; Inteligensia, Charles Mkumbo, Kamishna Msaidizi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo baada ya kikao kazi cha Maofisa wa Polisi kilichofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam hivi karibuni.
Maafisa wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kushoto) na Isaac Mgwassa (kulia) wakibadilishana mawazo na Kamishna Msaidizi; Tathmini na Ufuatiliaji, Semiyono.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, S.R. Handuni akifurahia jambo na Afisa wa Benki ya NMB, Amanda Feruzi.
BENKI ya NMB, imewahakikishia askari wa Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa Serikali nchini, huduma bora, rafiki na sahihi za kibenki, zitakazokuza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, ili kuendana na kasi ya maendeleo kuelekea Uchumi wa Kati.

Ahadi hiyo imetolewa na Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi na Kati wa NMB, Ally Ngingite, katika siku ya pili ya Kikao Kazi cha Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Mikoa na Vikosi, kinachofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages