A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, September 23, 2019

NBC yazindua mkopo wa bima

Waziri wa Ujenzi, na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele (kushoto), akizungumza na MKurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (wa tatu kushoto), mara baada ya mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wamiliki wa Malori  Tanzania (TATOA), ambako benki hiyo ilizindua rasmi huduma yake mpya ya mkopo wa bima.  Wanaoangalia ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo.


BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua mkopo wa bima ikiwalenga zaidi wafanyabiashara walio katika sekta ya uchukuzi.

Akizungumza na washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru alisema mkopo huo unapatikana kwa kuanzia kiasi cha shilingi milioni 1 mpaka milioni 300.

Alisema mkopo wa bima wa NBC ni kwa ajili ya bima za biashara zote zikiwemo biashara za magari, bidhaa zilizo safarini, majanga ya moto, ujambazi, hatari zote za barabarani na ajali kwa wafanyakazi.

“Mtu yoyote mwenye mahitaji ya bima akiwa na rasilimali zozote kama vile nyumba ana sifa ya kupata mkopo huu bila kuwa na dhamana yoyote.

“Utalipia miezi miwili ya bima yako NBC na sisi tutalipia miezi 10 inayobaki kwa wakala wa kwa niaba yako, nawe utailipa benki kila mwezi kidogo kidogo. Mkopo huu una riba ndogo kabisa kuliko mikopo yote inayotolewa na benki”, aliongeza Bwana Ndunguru.

Pamoja na hayo mkurugenzi huyo alisema, uamuzi wa kuanzisha huduma inayowalenga wafanyabiashara imetokana na kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano katika kuondoa kero zikizokuwa zikiizorotesha sekta ya uchukuzi.

“NBC imeongeza kutoa mikopo zaidi katika sekta ya usafirishaji, mkopo wa bima kutoka NBC unakuwezesha kuendelea kuikinga biashara yako dhidi ya hasara au matatizo mengine yoyote hata kama huna fedha taslimu za kulipia bima”, alisema.

Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa Ujenzi,  Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwele alipongea NBC katika juhudi inazofanya katika kuinua  sekta ya biashara ndogo na za Kati.




Akitoa mfano Waziri Kamwele alisema ni hivi karibu Benki ya NBC ilisaini makubaliano na Shirika la Posta Tanzania ambapo benki itaweka ofisi katika kila palipo na tawi la Shirika hilo popote nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages