NA HERI SHAABAN(KINONDONI)
MANISPAA ya Kinondoni yatangaza mitaa 106 itakayoshiriki uchaguzi Serikali za Mitaa mwaka 2019.
Akitoa maelekezo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu katika halmashauri ya manispaa hiyo,Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Kiduma Mageni alisema kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 9 kanuni za uchahuzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati za Mtaa tangazo la Serikali la february mwaka huu kwa kuzingatia orodha ya Mitaa kama ilivyotangazwa.
ageni alisema anatoa maelekezo kuhusiana na uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati za mtaa uchaguzi utafanyika siku ya Novemba 24 mwaka huu.
"Uandikishaji wa wapiga kura utaanza Octoba 8 mwaka huu hadi Octoba 14 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni katika mitaa 106 kata 20 katika vituo vya uandikishaji " alisema Mageni.
Mageni alisema uchaguzi utafanyika kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni katika vituo vilivyopangwa katika kila mtaa amewataka wananchi kupita katika ofisi za Ofisa Mtendaji Kata kwa ajili ya kupata elimu kuhusiana na uchaguzi huo.
Aidha alisema fomu za kugombea nafasi za Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wake zitatolewa Octoba 29 hadi Novemba 5 mwaka huu na mwisho wa kurudisha fomu Novemba 5 katika ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi kila mtaa .
Pia alisema pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea litawashirishwa kwa maandishi kwa Msimamizi wa uchaguzi kwa muda wa siku mbili mara baada uteuzi kufanyika na msimamizi Msaidizi.
"Kamati ya Rufaa ya Wilaya itasikiliza rufaa dhidi ya uamuzi wa msimizi msaidizi wa uchaguzi Novemba 5.mpaka 9 mwaka huu" alisema.
Akielezea kuanza kwa kampeni alisema kampeni itakuwa siku saba kabla ya siku ya uchaguzi Novemba 7 hadi 23 katika mitaa yote ya uchahuzi .
Aliwataka wananchi wa Wilaya ya Kinondoni wapige kura katika vituo walivyojiandikisha vituo vyote vitafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi.
Alitaja baadhi ya mitaa Kata ya Kinondoni Mtaa wa Kumbukumbu ,Kino doni Mjini,Kinondoni shamba,Kata ya Makumbusho ,Ada Estate,Mchangani,Mbuyuni,Minazini,Kisiwani,Sindano,Makumbusho.
No comments:
Post a Comment