A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, August 25, 2019

upo tayari na tunataka kushinda - Kocha Mkuu wa Simba SC

Kocha wa Simba SC, Patrick Aussems amesema wanajua wanatakiwa kushinda na watafanya hivyo katika mchezo wa marejeano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kati ya Simba dhidi ya UD Songo ya Msumbiji,

Ameyasema hayo kwenye mkutano na wanahabari uliohusisha makocha wa timu zote mbili, ambapo mbali na ushindi amesema kikosi chake kipo salama.

“Tupo tayari na tunajua tunataka kushinda, tutafanya kila kitu kufanikisha hilo na wachezaji wanajua hilo. Tunatakiwa kuwa makini, tunajua tunakutana na timu nzuri na utakuwa mchezo mgumu lakini tunajiamini'', Patrick Aussems.

Ikumbukwe Simba SC inahitaji ushindi wa aina yoyote katika mchezo huo kutokana na suluhu iliyopata ugenini wiki mbili zilizopita, kupoteza au sare yoyote ya magoli kutaindosha timu hiyo kwenye michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages