Katika maisha ya mwanadamu, suala ndoa ni jambo la muhimu sana linalomfanya atimize lile agizo la Mungu pale katika bustani ya Eden, Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”
Richard Seugata kutoka Amani, Tanga ni moja ya vijana walioamua kutimiza agizo hili la Mungu na kumtafuta mwenzi wake wa maisha mwaka 2015, lakini shetani alivyo mbaya tangu alipofunga ndoa mwaka huo wa 2015 alikaa muda mrefu akisubili mtoto lakini hakukua na matumaini yoyote ya kupata mtoto.
Katika hali ya kawaida ya maisha ya mwafrika Richard alikwenda kwa waganga wengi ndani ya wilaya ya muheza na wilaya za karibu kama Handeni na Pangani bila mafanikio. Wapo waliomshauri aende hospitali pamoja na makanisa mbalimbali lakini hakupata msaada bali changamoto ilikua inazidi kwakua mafarakano yalikua yanazidi kwenye familia, alisema Richard. Siku moja katika hali ya kutafuta chaneli za dini katika King’amuzi cha Dish (Free to Air Dish, IS20 Frequency Namba 12603) Alifanikiwa kuiona WRM TV akiwa nyumbani kwake Tanga, ambayo baada ya kuifuatilia akavutika kuja kushiriki Ibada ya maombezi na Unabii zinazoongozwa na Chief Prophet Nicolaus Suguye na kufanikiwa kufika Kanisani ambapo alitamkiwa neno la kinabii na Prophet Nicolaus Suguye kuwa watakwenda kuzaa mpaka watatamani kufunga uzazi.
Richard anashuhudia kuwa baada ya kutoka kanisani hapo WRM Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga Dar es Salaam mwezi mmoja baadaye mke wake alipokea ujauzito na tarehe 28.9.2018 alipokea zawadi ya mtoto wake wa kwanza, sina na utukufu anamrudishia Mungu wa Nabii Nicolaus Suguye, kwani amemuokoa katika aibu aliyokuwanayo kwa takribani miaka 3 bila uzao.
No comments:
Post a Comment