Mkurugenzi wa Halmashauri ya,Ilala Jumanne Shauri akisoma taarifa katika uchaguzi wa Naibu meya wa Ilala leo.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Ojambi Masaburi akizungumza katika Baraza la madiwani
NA HERI SHAABAN(ARNATOGLUO)
CHAMA CHA MAPINDUZI ( CCM ) Wilaya ya Ilala imekibwaga chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)katika nafasi ya Naibu Meya Ilala.
Katika uchaguzi huo
CCM walimsimamisha Ojambi Masaburi aliyeibuka kidedea kwa kula 33 dhidi ya ya Elen Ryatula wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA aliyepata kula 21.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi wa Uchaguzi Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Jabir Makame alisema wajumbe jumla 57 wapiga kula waliopiga 54 akuna kula iliyoharibika katika uchaguzi huo.
Makame alisema uchaguzi ulikuwa tulivu.
Akizungumza katika uchaguzi huo mara baada kuteuliwa Naibu Meya Mteule Manispaa ya Ilala Ojambi Masaburi alipongeza wapiga kula wake kwa kumchagua kushika wadhifa huo.
Masaburi alipongeza viongozi wa CCM Wilaya kwa kumteua kwa kumpa tiketi ya CCM kugombea kiti hicho.
"Nashukuru kwa ushindi mnono madiwani wenzangu wa CCM kunichagua katika kiti hichi pia nawapongeza UKAWA kwa kunipigia kula madiwani watano yote ni mapenzi ya chama cha mapinduzi CCM katika utekelezaji wa Ilani Rais wetu John Magufuli" alisema Ojambi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Jumanne Shauri ,awali alifungua kikao cha Baraza la madiwani Ilala alisema kikao hicho ni cha kawaida ,uchaguzi wa Naibu Meya kila baada ya mwaka mmoja .
Mkurugenzi Shauri alisema wapiga kura wajumbe wa kuteuliwa au kupiga kuratatibu Meya Mwenyekiti,Mkurugenzi Katibu utaratibu wa ushindi wa kiti mgombea anatakiwa kupat kura zaidi zilizopigwa na wajumbe.
Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto alichagua kamati zake za kufanya nao kazi ,Kamati za Mipango Miji na Mazingira na Kamati na Kamati za Huduma za Jamii.
No comments:
Post a Comment