Aidha amemshukuru Rais Magufuli kwa kuweza kupigania hoja ya Lugha ya Kiswahili kuingia katika Lugha Nne zinazotumiwa katika Jumuiya ya SADC na kuwahimiza Walimu, Baraza la Kiswahili Tanzania na wataalamu wa kiswahili kuchukulia hatua hiyo kama fursa ya ajira.
Hata hivyo amewataka Wafanyabiashara na wanachi kuchangamkia fursa za Kibiashara zinazopatikana katika nchi wanachama ikiwemo Fursa ya kuuza Vyakula na mazao.
Pamoja na hayo amewashukuru Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam kwa ukarimu na utulivu walioonyesha kwa kipindi chote cha Ugeni wa SADC jambo lililowezesha Wageni Kuingia nchini salama na kuondoka salama.
No comments:
Post a Comment