Wakati Taifa linajiandaa kwenda katika Uchaguzi wa Viongozi wa
Serikali za Mitaa, Wito umetolewa kwa wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao
ya msingi kwa kupiga kura za kuchagua Viongozi wenye hofu ya Mungu na wanaojali
haki za Watoto wa Kike.
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Shirika la utetezi wa haki za
mtoto wa kike la New Hope Tanzania Bi. Elizabeth Ngaiza ambapo amesema Katika
Kampeni ya "Niache Nisome Kwanza" anayoendesha amebaini uwepo wa baadhi
ya viongozi wa Ngazi za mitaa wasiokuwa na weledi, wasiowajibika na hawawezi
kusimama katika nafasi yao kutetea haki za mtoto wa kike.
Aidha Bi. Elizabeth Ngaiza amesema lengo la Kampeni ya
"Niache Nisome Kwanza" ni kupambana na mimba za utotoni kwa mtoto wa
kike na kuhakikisha anawekewa mazingira wezeshi ya kusoma pasipo changamoto
wala vikwazo vyovyote.
No comments:
Post a Comment