A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, July 20, 2019

Marekani kutuma wanajeshi Saudi Arabia

Maafisa wa Marekani wamesema leo kuwa nchi hiyo inatuma mamia ya wanajeshi pamoja na ndege za kivita na mifumo ya ulinzi nchini Saudia Arabia ili kukabiliana na Iran.

Maafisa hao wamesema, hatua hiyo imekuwa ikifanyiwa kazi kwa wiki kadhaa na haikuchochewa na kisa cha Iran kuikamata meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la Ghuba jana Ijumaa.

Baadhi ya wanajeshi tayari wamewasili kwenye kambi ya kijeshi ya Prince Sultan kusini ya mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh na watakuwa na jukumu la kusimamia ulinzi.

Saudi Arabia imesema mpango huo unalenga kuimarisha usalama wa kanda hiyo na kulingana na maafisa wa Marekani idadi ya wanajeshi wanaotumwa inaweza kupindukia 500.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages