A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, July 20, 2019

Iran kuichunguza meli ya mafuta ya Uingereza iliyoikamata

Iran imesema leo kuwa imefungua uchunguzi dhidi ya meli ya mafuta inayopeperusha bendera ya Uingereza ambayo iliikamata jana Ijumaa ikidai kuwa iligongana na meli ya uvuvi kwenye mlango bahari wa Hormuz.

Kikosi cha Ulinzi wa Mapinduzi cha Jeshi la Iran, kimesema kiliikamata meli iitwayo 'Stena Impero' kwa kukiuka kanuni za kimataifa za usafiri wa bahari katika ujia wa Hormuz, eneo muhimu linalopitisha karibu theluthi ya mafuta ghafi duniani.

Uingereza imesema Iran imezikamata meli zake mbili za mafuta kwenye eneo la Ghuba na waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo Jeremy Hunt alionya kuwa watachukua hatua nzito iwapo suala hilo halitotatuliwa haraka.

Mmiliki wa meli ya pili iitwayo 'Mesdar' aliarifu kuwa chombo hicho kilishikiliwa kwa muda na watu wenye silaha kabla ya kuachiwa huru na kuruhusiwa kuondoka.

Matukio hayo yamejiri saa chache tangu mahakama ya Gibraltar kusema inarefusha kwa siku 30 kushikiliwa kwa meli ya mafuta ya Iran iliyokamatwa wiki mbili zilizopita kwa madai ya kuikuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Syria.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages