A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, June 10, 2019

Undertaker amshushia kipigo kizito Goldberg

Usiku kuamkia Jumamosi ya wikiendi iliyomalizika, mwanamieleka William Calaway maarufu kama Undertaker amemcharaza mpinzani wake William Scott maarufu kama Goldberg katika mchezo wa Super Showdown nchini Saudi Arabia.

Awali kabla ya mchezo huo, tambo za wababe hao zilivuta hisia za mashabiki wengi kutokana na rekodi za wawili hao katika medani ya mchezo huo wa mieleka.

Mchezo huo ulidumu kwa dakika 24, Undertaker akipigwa mara tatu lakini haikufanya kumzuia Undertaker kuibuka mshindi wa pambano hilo.

Matokeo mengine, Randy Orton amemshinda Tripple H, Braun Strowman amemtandika Bobby Lashley huku bingwa wa WWE Kofi Kingston ametetea ubingwa wake dhidi ya Dolph Ziggler.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages