A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 25, 2019

Simba SC wasajili mwingine kutoka Brazil

Klabu ya Simba imemtambulisha mchezaji mwingine kutoka Brazil, Gerson Fraga Vieira (26), ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo akitokea klabu ya ATK ya India.

"Mchezaji mwingine kutoka Brazil mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji, Gerson Fraga Vieira (26) amesaini mkataba wa miaka miwili na Mabingwa wa nchi," imeeleza taarifa ya klabu hiyo.

"Vieira ambaye amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 17 ya Brazil iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Alisson, pia alicheza timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 20 na alicheza klabu kadhaa za Brazil ikiwepo Grêmio amejiunga na klabu yetu akitokea ATK FC ya India" ameeleza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages