Mkuu wa Mkoa wa Dar es Mhe. Paul Makonda, akizungumza wakati wa
hafla ya kugawa vyakula kwa ma imamu kutoka katika misikiti zaidi ya 1000
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Mhe. Paul Makonda, akikabidhi chakula kwa
mmoja wa maimamu waliofika katika hafla ya kugawa vyakula kwa ma imamu zaidi ya misikiti1000 wa jiji hilo. Kushoto kwa mkuu wa mkoa ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa kata
ya Vingunguti Omary Kumbilamoto, na wengine ni wawakilishi kutoka ubalozi wa
Falme za Kiarabu pamoja na sheikh mkuu wa Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ahmad Mussa (kulia),
akisalimiana na Balozi Mdogo kutoka Falme za Kiarabu wakati wa hafla ya Mkuu wa
Mkoa Paul Makonda kutoa msaada wa vyakula kwa masheikh wa mkuo huo leo. (Katikati)
ni Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Mhe. Paul Makonda leo amewakabidhi shehena
ya viungo vya kutengeneza futari kwa maimamu,
mashehe na viongozi wa Dini ya Kislamu kutoka Misikiti zaidi ya 1,000 kama
sehemu ya sadaka na shukrani ya Amani na Utulivu ndani ya mkoa huo.
Miongoni mwa vitu alivyokabidhi RC Makonda ni Mchele, Sukari,
Unga, Maharage, Mafuta na vitu mbalimbali kwaajili ya kuwawezesha viongozi
hao kufurahia futari majumbani mwao.
RC Makonda amewashukuru viongozi wa dini kwa kuwa
wasimamizi wazuri wa Amani na mshikamano
ndani ya mkoa huo jambo linalofanya mkoa huo kuendelea kuwa kisima cha Amani.
Hata hivyo RC Makonda amewaeleza
Viongozi wa Dini kuwa namna bora ya kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli na
kumuombea ni kuhakikisha waumini wao wanajiandikisha kwenye daftari la kudumu
la wapiga kura ili wachague viongozi wa serikali za mitaa wanaochukia Rushwa.
Aidha RC Makonda amemshukuru Balozi wa Falme za Kiarabu kwa kumkabidhi
misaada hiyo huku akiwasihi waislamu kutumia mfungo huu Kuliombea taifa na viongozi pamoja na kuwahimiza
wazazi kuwalea watoto katika malezi bora.
Kwa upande wake Balozi mdogo wa
Falme za Kiarabu amesema wameamua kumuunga mkono RC Makonda kwakuwa wanamuamini
akipokea kitu kinawafikia walengwa na amekuwa mtu wa kuwasaidia watu
wasiojiweza bila kujali dini wala kabila.
No comments:
Post a Comment