A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, March 22, 2019

WATALAAM NCHI ZA SADC WAKUTANA DAR KUJADILI NA KUWEKA MUONGOZO MFUMO WA UNUNUZI DAWA WA PAMOJA KUPITIA MSD

 Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WATALAAM wa sekta ya afya na hasa katika upande wa ununuzi wa dawa kutoka nchi za SADC wamekutana nchini Tanzania kwa lengo la kujadili pamoja na kutoa muongozo  utakaosaidia kufanikisha mfumo wa ununuzi wa dawa kwa pamoja kwa nchi hizo.

Jukumu la kununua na kusambaza dawa hizo kwa nchi za SADC limekabidhiwa kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) nchini ya Tanzania baada ya kukidhi vigezo na sifa ambazo zilikuwa zimewekwa na nchi hizo.

Akizungumza leo Machi 21,2019 jijini Dar es Salaam Mgeni rasmi wa mkutano huo wa watalaam wa sekta ya afya kwa nchi za SADC na hasa upande wa manunuzi ya dawa, Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi amesema mkutano huo ni muhimu kwani utatoa muongozo wa namna bora ya kufanikisha ununuzi wa dawa wa pamoja.

Amesema jukumu la kununua dawa hizo na kuzisambaza kwa nchi za SADC lipo kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na hivyo kabla ya kuanza kwa utaratibu huo watalaam wamekutana kuweka mkakati utakaofanikisha ili kufikia lengo.

 "Hiki nikao cha kitalaam ambacho lengo lake ni kujadili namna bora ya kufanikisha ununuzi wa dawa kwa pamoja.Pia ni kikao kitakachotoa muongozo ili kufanikisha mfumo huo ambao ni mpya ingawa kwa nchi nyingine duniani wamekuwa wakiutumia kwa baadhi ya dawa,"amesema.

Kuhusu lini mfumo huo utaanza, Msasi amejibu utaanza baada ya kikao hicho cha watalaam kujadiliana na kwa upande wa MSD ipo tayari kwani walishajipanga kwa kazi hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD Abdul  Mwanja amesema wao wamejipanga na wako tayari kuanza kazi hiyo  ya ununuzi wa dawa wa pamoja ambao faida ya nyingi na kubwa utasaidia kukunua dawa kwa bei nafuu.

"Mnaponunua dawa kwa pamoja, wenye viwanda vya kuzalisha dawa watapunguza bei na hivyo kumuwezesha mwanchi anayehitaji dawa kuzipata kwa gharama ya chini. Hivyo ni mfumo ambao utasaidia nchi hizo kununua dawa wa gharama ya chini,"amesema.

Alipoulizwa kuhusu MSD wamewezaje kuaminiwa na kupewa jukumu hilo, amejibu kulikuwa na vigezo ambavyo viliwekwa na kazi nzuri ambayo imefanywa na MSD ikiwemo ya kusambaza dawa katika hospitali zote nchini Tanzania imewapa nafasi ya kupewa kazi hiyo.

Kuhusu changamoto za mfumo huo,amesema kwa sasa ni mapema mno maana bado hawajaanza , hivyo iwapo zitajitokeza wataangalia namna ya kukabiliana nazo lakini kwa namna ambavyo wamejipanga wana matumaini watatimiza jukumu hilo kikamilifu."Na kwa uwekezaji ambao umefanyika MSD inaweza kuifanya kazi hiyo kwa miaka mitano."


Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa MSD miaka miwili iliyopita walikuwa wananunua dawa kwa wazalishaji wa dawa 10 lakini sasa hivi wananunua kwa wazalishaji  148 ambao wameingia nao mkataba."Hii  itasaidia kupata dawa kwa gharama nafuu kwani hakuna mtu wa kati tena na tumekubaliana kila nchi itakuwa na fedha zake lakini anayenunua kwa niaba ya nchi hizo ni MSD."
Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kufungua mkutano wa kujadili mwongozo wa huduma ya ununuzi wa pamoja wa dawa kupitia kupitia MSD.

 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa wataalamu kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo (SADC)wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam leo ili kujadili mwongozo wa huduma ya ununuzi wa pamoja wa dawa kupitia MSD. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages