Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Serikali imesema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika Sekta ya afya wameweza kupunguza vifo vya wamama wajawazito kwa asilimia 40.
Hayo ameyasema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akifungua jengo la Huduma za Afya Binafsi katika Hospitali ya CCBRT, amesema kuwa vifo vya akina mama vilikuwa vingi kutokana na kukosekana kwa baadhi ya huduma lakini sasa Serikali imejenga vituo vya Afya 350 ikiwa pamoja na kuweka huduma za dharula ya kumtoa mtoto tumboni.
Amesema kuwa CCBRT imekuwa ni moja ya Hospitali iliyoweza kupambana na ugonjwa wa Fistula ambao ilikuwa unafanya wanawake kukosa amani. Mwalimu amesema serikali imeondoa kodi katika dawa, vifaa tiba pamoja na vitendanishi ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa gharama nafuu. Aidha ameiagiza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kulipa kwa wakati madai ya watoa huduma za afya ili fedha hizo ziweze kuendesha huduma mbalimbali ikiwemo kulipa mishahara ya watumishi.
Amesema wagonjwa asilimia 60 wanatibiwa kwa msamaha hivyo huduma za wagonjwa binafsi ndio wanaweza kuchangia katika kuziba sehemu ya huduma kwa wale wasio na uwezo. Amesema kwa CCBRT kujenga jengo kwa ajili ya a wagonjwa binafsi wataongeza huduma mapato pamoja kuendelea kutoa huduma kwa wale wasiojiweza.
Nae Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT Brenda Msangi amesema kuwa ilianza kwa kutoa huduma za macho lakini kutokana kuzidi kuimarika walianzisha huduma zingine kufikia kujenga jengo la wagonjwa Binafsi. Amesema kuwa CCBRT mipango yake ni kuhakikisha wanawafikia wananchi wote katika utoaji wa huduma za afya zilizo bora.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la wagonjwa binafsi katika hospitali ya CCBRT.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipata Maelezo kutoka Kwa Dkt. Luijisyo Mwakalukwa kuhusiana Idara ya Mifupa na Utengamao inavyofanya kazi wakati Waziri huyo akitembelea maonesho katika uzinduzi wa Jengo la Wagonjwa Binafsi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipata maelezo kutoka kwa Muuguzi Mwandamizi Idara ya Macho wa CCBRT Neema Manyerere wakati Waziri huyo akitembelea maonesho katika uzinduzi wa Jengo la Wagonjwa Binafsi katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Brenda Msangi akitoa maelezo kuhusiana na Jengo la Wagonjwa Binafsi katika katika uzinduzi wa Jengo la Wagonjwa Binafsi katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na hadhara ya Hospitali ya CCBRT mara baada ya kufungua Jengo la Wagonjwa Binafsi katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam.
Vifaa Bandia wanaowekea katika Hospitali ya CCBRT
No comments:
Post a Comment