Mapenzi yana kanuni zake, kanuni ambazo usipozifuata huwezi kupata
furaha uliyotarajia. Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza
lakini omba sana upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda
kwa dhati.
Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu ambaye wala hana hata chembe za
penzi kwako, utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa
unajitafutia vidonda vya tumbo.
Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata wapenzi wa ukweli lakini kwa
kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii
wameachika na bado wanaranda mtaani.
Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na mtu na ukabaini naye
anakupenda, hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia utundu na ubunifu
wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa pekee
kwake.
Ninapozungumzia hayo, namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi ambayo
hakika nikianza kuyaelezea hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo
nigusie utundu katika uwanja wetu ulee wa kujidai.
Faragha ni eneo muhimu sana ambalo linaweza kubomoa au kuimarisha ndoa. Ninapozungumzia hilo, ni kwa wote yaani mke na mume.
Mwanaume anatakiwa kumridhisha mkewe kwa kiwango kinachostahili.
Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo kiduchu kwani ikiwa hivyo lazima mke
atakosa furaha iliyokamilika.
Ila sasa leo nataka niwazungumzie kwa kirefu wanawake. Kuna wanawake
ambao wamebahatika kupata wanaume wanaowapenda sana na kuwapatia kila
wanachohitaji.
Hawa wanatakiwa kujiona ni wenye bahati kubwa kwani kwa hali ilivyo
sasa, wanawake wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa hawawapati.
Kinachonishangaza ni kwamba, kuna baadhi ya wanawake ambao wako ndani ya
ndoa lakini wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa waume zao furaha
ambazo hawawezi kuzipata kwingine.
Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake wengi walio ndani ya ndoa siku
hizi wanasalitiwa sana. Hii ni kwa sababu wamekuwa waongeaji sana lakini
wanapokuwa faragha unaweza ukadhani siyo wao. Hawajui kitu, wamekaa
kama magogo tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa na ndoa zao zitadumu,
zitadumu kwa misingi ipi?
Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni kama mtoto ambaye anatakiwa
kubembelezwa huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza asishawishike
kutoka nje. Ukiwa kwenye ndoa kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa
kuwa tayari ulishapendwa ipo siku utajikuta ni mke wa pambo la nyumba
tu.
Mtaani kuna utitiri wa nyumba ndogo, wanaume walioanzisha makoloni hayo
nje ya ndoa zao walikosa wake sahihi ambao wanaweza kuwashikilia waume
zao.
Matokeo yake sasa nyumba ndogo hizo ndizo zinazooonekana kuwashika waume
za watu siku hizi na wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na wabunifu.
Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye ndani ya ndoa usifanye kama yale
wanayofanya nyumba ndogo? Kuna dada mmoja nilizungumza naye hivi
karibuni akaniambia eti amenuniana na mumewe huu ni mwezi wa pili baada
ya mwanaume wake huyo kutaka afanyiwe mambo ambayo yeye aliona kinyaa
kuyafanya.
Kabla ya kumjibu kwanza niliguna, sababu ya kuguna ni kwamba
niliyagundua hayo mambo ambayo aliona kinyaa kumfanyia mumewe. Niseme tu
kwamba, mapenzi wakati mwingine ni uchafu, wanaojua mapenzi wanajua kwa
nini nasema hivyo.
Nilichomjibu mwanamke huyo ni kwamba, kama mwanaume huyo anampenda
amfanyie kila atakacho isipokuwa kukubali kufanya mapenzi kinyume na
maumbile na nikamwambia kuwa, mapenzi ni uchafu hivyo hayo ambayo anaona
kinyaa kumfanyia mumewe ndiyo ambayo wengine wamekuwa wakiyafanya na
wamefanikiwa kuzishika ndoa zao.
Naomba niseme tu kwamba, huenda unajiamini kuwa ni mzuri na umbo la
kuvutia kiasi kwamba, ni rahisi kupata mwanaume wa kuoa lakini tambua
bado utakuwa na kazi kwenye kuidumisha ndoa na kuhakikisha hukaribishi
mazingira ya mumeo kutafuta nyumba ndogo.
Hakikisha unaonesha uanamke wako ili hata kama huyo mumeo atatoka nje,
iwe ni kwa tamaa zake tu lakini mambo ya msingi uwe unampatilizia.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, March 14, 2019
Mwanamke anachotakiwa kufanya mume asitoke nje ya ndoa
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment