Taasisi inayojihusisha na utafiti wa masuala ya anga nchi Marekani NASA
imetangaza kwamba binadamu wa kwanza atakayekanyaga katika sayari ya
Mihiri "Mars" anaweza akawa mwanamke .
Rais wa NASA Jim Bridenstine,akiongea katika kipindi kimoja cha redio
alichoshiriki alisema kuna uwezekano binadamu wa kwanza atakayekanyaga
katika sayari ya Mihiri akawa mwanamke.
Bridenstine alisema bado haijaamuliwa ni mtu gani ataenda katika sayari
ya Mihiri, alifahamisha kwamba mipango yao kwa siku zijazo ni
kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu na kuwa mstari wa mbele.
Bridenstine, alimjibu shabiki mmoja aliyemuuliza kupitia mtandao wa
kijamii wa Twitter kama katika safari ya mwezi ujao ya NASA kutakuwa na
nafasi kwa wanawake , kwa kusema “bila shaka”
NASA kwa mara ya kwanza ipo katika maandalizi ya kumpeleka mwanamke katika anga za mbali.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, March 14, 2019
Binadamu wa kwanza kukanyaga katika sayari ya Mihiri "Mars" anatarajiwa kuwa mwanamke
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment