Na. John Walter,Babati
Mchungaji Emmanueli wa kanisa la Jesus Life Assemblies lililopo kitongoji cha Qatabradik anayeshutumiwa kutumia nguvu za Free Mason amemuomba Rais John Magufuli kumsaidia kujenga kanisa na waumini wamemkingia kifua wakikanusha tuhuma hizo.
Ombi hilo alilitoa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Nipashe eneo ambalo anatoa huduma ya kiroho ya kuombea watu na kuubili katika jirani na barabara ambapo anadai ameomba kwa muumini wake.
Mchungaji Tsino alisema kuwa yeye hatumii nguvu za free mason kama watu wa jamii ya pale wanavyosema badala yake anadai anatumia eneo la mungu ambalo limekuwepo siku zote hivyo hana chochote anachokitumia.
“Ninamuomba Rais wangu John Magufuli anisaidie kupata eneo la kujenga kanisa na anisaidie kujenga ili niendelee kumuombea na kuwaombea watu wengine ambao wana shida kama ambavyo nafanya hapa,’’Alisema Tsino
Aidha alisema toka aanzishe huduma hiyo kumekuwepo na maneno ya kumpiga kashfa kua ni free mason ila yeye anasema aliamua kufikisha injili maeneo ya vijijini ambako watumishi wengi wa mungu hawafiki ili watu wa vijijini waweze kusaidika.
Mmoja wa waumini wake Lucy Peter akizungumza na Nipashe alipinga mchungaji huyo kutumia nguvu za free mason huku akidai alifika kanisani hapo alikua amepooza ulimi na mikono alimuombea bila kutumia kitu chochote na alipona na mpaka sasa anaendelea na shughuli zake.
Beatha Pius naye ni muumini wa kanisa hilo ambaye amemkingia kifua mchungaji huyo na kukanusha tuhuma za free mason anazoshutumiwa mchungaji wake huku akisema alimuombea akapona ugonjwa wa kifua aliokua amezunguka Hospitali nyingi bila mafanikio na anampongeza amewaombea vijana wameacha pombe.
Mzee Tsolo Fisoo alisema mchungaji huyo anawaombea watu wengi wanapona na vijana wameanza kubadirika ila kusema ni Free Mason hizo ni fitina za watu wa madhebu mengine wanaolenga mkufitini asiendelee.
Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Qatabradik Rubanus Slaa alisema wao kama serikali wamempokea vizuri akiwa na vielelezo vyote vya usajili wa kanisa lake huku akisema huduma anayoifanya inaisaidia serikali kukomesha vitendo vya kiharifu na akadai amewabadirisha vijana waliokuwa walevi.
No comments:
Post a Comment