A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 18, 2019

Kijana aliyesambaza kanda ya video ya shambulizi la misikiti afunguliwa mashitaka


Kijana wa miaka 18 amefunguliwa mashitaka mjini Christchurch nchini New-Zealand kwa sababu ya kusambaza mubashara kanda ya video mtandaoni inayoonyesha mashambulio dhidi ya msikiti Al Noor.

 Anakabiliwa pia na mashtaka ya kuchapisha picha ya msikiti huo pamoja na kuandika "Lengo limefikiwa na pia kwa kushangiria matumizi ya nguvu".

Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 14 jela kwa kila kosa moja. Watu 50 wameuwawa kufuatia mashambulio katika misikiti miwili ya mji wa Christchurch nchini New-Zealand na wengine 50 pia kujeruhiwa.

Mtuhumiwa Brenton Tarrant anasema atajitetea mwenyewe mahakamani. Kwa mujibu wa polisi, raia huyo wa Australia hakusaidiwa na mtu yeyote katika kuandaa na kufanya mashambulio hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages