Meneja Uendelezaji Biashara na Masoko wa Kampuni ya bima ya UAP Old Mutual Tanzania , Jabir Kigoda ( wa tatu kulia) akikabidhi sehemu ya mifuko 400 ya shule kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk. Ave Maria Semakafu ( wa nne kushoto) , iliyotolewa na UAP kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu katika hafla iliyofanyika Muheza, Tanga, hivi karibuni. Anayeonekana nyuma ya Naibu Katibu Mkuu ( mwenye hijab) ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo akiongea katika hafla hiyo ya makabdhiano.Kulia kwake ni Meneja wa Uendelezaji Biashara na Masoko wa UAP Jabir Kigoda, na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr. Ave Maria Semakafu.
Meneja Uendelezaji Biashara na Masoko wa Kampuni ya bima ya UAP Old Mutual Tanzania , Jabir Kigoda ( wa tatu kulia) akikabidhi sehemu ya mifuko 400 ya shule kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk. Ave Maria Semakafu ( wa tatu kushoto) , iliyotolewa na UAP kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu katika hafla iliyofanyika Muheza, Tanga, hivi karibuni. Anayeonekana nyuma ya Naibu Katibu Mkuu ( mwenye hijab) ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo
Watoto wenye mahitaji maalum wakiwa kwenye picha ya pamoja na naibu katibu mkuu, mkuu wa wilaya na viongozi wa UAP baada ya kupokea msaada.
Watoto walio na
mahitaji maalum Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga hivi majuzi walipatiwa msaada wa mifuko
400 ya shule na kampuni ya bima ya UAP
Old Mutual Insurance Tanzania, ikiwa ni
kutimiza azma ya kampuni hiyo ya kutoa misaada kwa kundi hilo la watoto.
Msaada huo, wenye
lengo la kunyanyua ushiriki wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum, ulitolewa
na Meneja Uendelezaji Biashara na Masoko wa UAP katika hafla iliyofanyika
Muheza, huku ukipokelewa kwa niaba ya
walengwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr. Ave
Maria Semakafu .
“ Sisi katika
kampuni ya UAP tunaamini kuwa elimu siyo tu ni nguzo ya mafanilkio ya binadamu, bali pia ni
haki ya msingi ya mtoto, wakiwemo watoto wenye mahitaji maalum kama hawa, ”alisema
Kigoda wakati wa kukabidhiana msaada huo.
Vilevile Kigoda alichukua
fursa hiyo kuwaasa wadau katika sekta mbalimbali nchini kuwa mstari wa mbele katika
utoaji wa misaada kama hiyo, kwa kuwa
siyo tu itawawezesha watoto bali itachagiza harakati za utekelezaji wa sera ya taifa
ya elimu bure.
Kampuni ya UAP,
yenye matawi maeneo mbalimbali nchini ikiwamo Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma,
Kahama, Zanzibar, Morogoro and Mtwara,ni moja kati ya makampuni ambayo yameweka
kipaumbele katika kuwekeza kwenye misaada ya kuchangia maendeleo ya jamii.
No comments:
Post a Comment