A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, February 11, 2019

Dkt. Mwigulu Nchemba aeleza sababu za ukimya wake

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema kwa sasa amekuwa kimya kutokana hayopo tena kwenye nafasi hiyo, hivyo amekuwa na vitu vichache vya kusemea.

Ameeleza hayo kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 kinachoruka Clouds TV amesema kwa sasa amekuwa zaiddi jimboni kwake.

"Unajua ukiwa kwenye nafasi ya uwaziri vipo vitu vingi vya kuvisemea, ndio maana sasa hivi nipo kimya nimebaki na vitu viwili tu vya kusemea mambo ya jimboni kwangu na kazi nzuri inayofanywa na serikali yangu," amesema Dkt. Mwigulu.

Ameendelea kwa kusema, 'Hakuna tofauti na maisha yangu hayajabadilika, nilipokuwa waziri kwenye msafara wangu sikutaka magari yasimamishwe ili nipite, kwa sababu kuna wengine walikuwa wanawahi ndege "airport', wengine wagonjwa na wengine makazini sikutaka kuwachelewesha,'.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages