A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, February 28, 2019

BISHOP DKT LWAKATALE AANDAA TAMASHA KUBWA LA WANANDOA

Askofu Dkt. Getrude Lwakatare.

Kanisa la Assemblies of God, lililopo Mikocheni B kwa Askofu Dkt. Getrude Lwakatare limeandaa Tamasha kubwa la Usiku wa Wanandoa lililopewa jina la MARRIAGE REVIVAL PART.

Akizungumza na Global Tv online Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Askofu Dkt Getrude Lwakatare alisema kuwa Tamasha hilo litafanyika March 8, mwaka huu katika kanisa la Asemblies of God lifahamikalo kama Mlima wa Moto lililopo Mikocheni B jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Dkt. Lwakatare alisema kuwa katika Tamasha hilo Wanandoa watapata wasaa wa kukumbushwa juu ya upendo wao na kuelekezwa namna ya kukaa vizuri kwa pamoja kwenye ndoa ambayo Mungu amewawezesha kuwa nayo.

Akifafanua zaidi Dkt. Lwakatare amesema Tamasha hilo halibagui Dini wala Dhehebu bali watu wote ambao ni wanandoa wa dini zote wanakaribishwa kuhudhuria Usiku huo wa Wanandoa.
Hata hivyo amesema kuwa Baadhi ya wanandoa watakaoonekana ndoa zao kuwa vizuri kulingana na vigezo vilivyopo watapata nafasi ya Kulala katika hoteli kubwa zenye hadhi ya Nyota tano(FIVE STAR) bure, huku wengine wakipata nafasi ya kupelekwa Saloon kubwa kwa ajili ya kupambwa kwa wanawake na wanaume kupelekwa saloon za Kiume.

Aidha amefahamisha kuwa kutakuwa na zawadi zingine mbalimbali zitakazotolewa kama vile Pesa, nguo mbalimbali kulingana na taratibu zilizopo pamoja na vigezo vilivyowekwa.

Tamasha hili la wanandoa limekuwa likifanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu Kiingilio Dkt Lwakatale amesema kitakuwa ni Tsh 30,000 ambapo mtu atapata fursa ya kupata chakula pamoja na vinywaji mbalimbali.
Tamasha hilo la wanandoa litapambwa na wachekeshaji mbalimbali pamoja na waimbaji wakiwemo Bahati Bukuku, Christina Shusho na wengineo bila kuwasahau wanenaji kwenye tamasha hilo ambao ni Irene Mbowe (KUNGWI) pamoja na Rev Daniel Mgogo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages