A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, January 16, 2019

Naibu Waziri wa Madini aagiza wafuatao kukamatwa na Polisi


Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameagiza kukamatwa kwa Wamiliki wa mgodi wa Nyakavangala kufuatia kutofautiana kuhusu taarifa waliyoiwasilisha kwa Naibu Waziri kuhusu namna mgodi huo unavyoendeshwa ikiwemo ulipaji wa kodi na mrabaha.

Alisema pamoja na kujionea shughuli za uchimbaji katika migodi ya dhahabu ya Ulata na Nyakavangala, amebaini ukwepaji mkubwa wa kodi pamoja na mrabaha wa serikali.

“Hatutaki ugomvi hapa kwenye migodi. Tunataka mgodi ufanye kazi. Dhahabu ziuzwe mahali panapoonekana. Hapa naona hesabu za viroba tu. Mnunuzi wa dhahabu hapa ni nani”, alihoji Naibu  Waziri.

Imeonekana kuwa kuwa mgodi huo unadaiwa zaidi ya Tsh. Milioni 128 za mrabaha ambazo imedaiwa kuwa, wapo baadhi ya wamiliki ambao wamekuwa wakikusanya fedha hizo lakini zimekuwa hazilipwi kwa serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages