A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, January 20, 2019

Kocha Yanga SC awajia juu waamuzi wa soka nchini

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera ameamua kuuwasha moto kwa Waamuzi wa Ligi Kuu Bara baada ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Stand United.

Kocha huyo ambaye timu yake ilifungwa kwa bao 1-0 huko Shinyanga ameeleza kuwa waamuzi wa soka la Tanzania wamekuwa na mapungufu mengi.

Zahera ameisifia Ligi ya Tanzania akiamini kuwa ni bora zaidi lakini akitupa lawama zake kwa baadhi ya waamuzi wanaoifanya ipoteze mvuto.

Hata hivyo amewashauri Viongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kujaribu kufuatilia mchezo wao wa jana walicheza na Stand ili kubaini madhaifu ya waliochezesha mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages