WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amempongeza Mufti wa Tanzania kwa namna ambavyo
uongozi wake umemaliza migogoro ambayo ilikuwa inaibuka kwenye misikiti
mbalimbali nchini na kwamba kwa sasa Waislamu ni wamoja.
Pia
Waziri Mkuu Majaliwa ametumia nafasi hiyo kuzungumzia hali ya amani
nchini ambayo msingi wake unatokana na viongozi wa dini zote ambao
wamekuwa wakihimiza umoja na mshikamano.
Majaliwa
amesema hayo jana mbele ya Rais Dk.John Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi
kwenye sherehe za BAKWATA kufikisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake
Desemba 17 mwaka 1968 ambapo amesema dini zote zimekuwa mstari wa mbele
katika kushiriki katika maendeleo nchini.
Ametumia
nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo Mufti wa Tanzania ambavyo chini ya
uongozi wake ambavyo amesaidia kuwafanya Waislamu nchini kuwa wamoja na
kushiriki kwenye maendeleo ya nchi yao.
"Leo
hii tunashudia chini ya Mufti wa Tanzania,hatusikii migogoro ambayo
tulikuwa tunaisikia siku za nyuma.Kumetulia na mambo yanakwenda
vizuri.Hongera Mufti Sheikh Aboubakary Zubeiry kwa uongozi wako
mahiri.Tangu uwe kwenye nafasi hiyo sasa ni mwaka wa tatu,umetuunganisha
," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Wakati
huo huo amezungumzi mchango wa viongozi wa dini zote pamoja na waumini
wa dini hizo kwa namna ambavyo wamekuwa wakishiriki katika kuleta
maendeleo ya nchi yao na kuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Magufuli
katika kuleta maendeleo.
Amesema"
Mchango wa viongozi wa dini zote wamekuwa mstari wa mbele katika
kushiriki kwenye maendeleo ya nchi yetu, kupitia taasisi zao mbalimbali
wamekuwa wakisaidia sekta ya afya, maji na utoaji wa huduma nyingine za
kijamii.Kabla
ya Waziri Mkuu kuzungumza Mufti wa Tanzania Sheikj Zubeiry alieleza
namna ambavyo sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali
BAKWATA ambao wamefika hapo.
Pia
amesema Mufti Zubeiry amesema BAKWATA limefurahishwa na uamuzi wa Rais
Dk.John Magufuli kukubali wito wao wa kuhudhuria sherehe za baraza hilo
kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Amesisitiza
kwamba viongozi wote wa BAKWATA nchini zima wako kwenye sherehe hizo za
kutimiza miaka 50, pamoja na viongozi wengine wa taasisi ya
dini,mabaraza ya dini pamoja na maimamu mbalimbali wamehudhuria sherehe
hizo.
"Viongozi
wote wako hapa kuqnzia ngazi ya wilaya hadi Taifa.kwa idadi ya
waliokuwepo leo tungeweza kusema ni kama mkutano mkuu kutokana na idadi
ya walioshiriki na nafasi zao," amesema Mufti Zubeiry wakati
anazungumzia sherehe hizo na aina ya viongozi waliohudhuria
No comments:
Post a Comment