Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MASHEIKH
wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania( BAKWATA) katika mikoa yote ya
Tanzania wamempongeza Sheikh Mkuu Aboubakary Zubeiry kutokanana namna
ambavyo amejenga umoja na mshikamano ndani ya baraza hilo.
Wametoa
kauli hiyo jana mbele ya Rais Dk.John Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi
kwenye sherehe za kutimiza miaka 50 ya BAKWATA tangu kuanzishwa kwake
Desemba 17 mwaka 1968.Akizungumza
kwa niaba ya masheikh wa mikoa, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad
Mussa Salum amesema wanampongeza wanampongeza Muft Zubeiry kwa namna
ambavyo amefanya mabadiliko makubwa ya kuwaunganisha Waislamu nchini.
"Wakati
leo tunasheherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa BAKWATA ,salamu za
kipekee tunazipeleka kwa Mufti wa Tanzania kwani maadhimisho hayo
yanamkuta yakiwa mikononi mwake."Chini
ya Mufti wetu Sheikh Zubeiry BAKWATA imekuwa mpya,na walio chini yake
tunapendana,tunaheshimiana na tunajitambua .Kupitia kauli mbiu yake ya
Jitambue, Mabadilaka,Acha mazoea hakika imetusaidia kutubadilisha na
kila mmoja wetu anajua majukumu yake," amesema Sheikh Alhad.
Amesisitiza
kupitia Mufti wa Tanzania BAKWATA imeunganishwa na walio chini yake
wamekuwa waaminifu na walio tayari kuhakikisha baraza hilo linasonga
mbele kimaendeleo.Pia
amesema kuwa BAKWATA kwa sasa wamekuwa na uhusiano mzuri na taasisi
nyingine na chini ya Mufti Zubeiry kuna maendeleo makubwa yanaendelea
kufanyika ukiwamo wa ujenzi wa msikiti mkubwa ambao unajengwa katika
makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam.
Wakati
huo huo Sheikh Alhad alitumia nafasi hiyo kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa
Dar as Salaam Paul Makonda ambaye hakusita kuelezea mafaniko ambayo
BAKWATA wameyapata kwa miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Amesema
amefurahishwa na viongozi wa dini zote Mkoa wa Dar as Salaam ambavyo
wanaishi kwa ushirikiano mkubwa huku kwa sehemu mkubwa wakijikita
kuhimiza umoja,amani na mshikamano miongoni mwa wananchi wote.
"Nitumie
fursa hii kulipongeza Baraza Kuu la Waislamu Tanzania kwa kutimiza
miaka 50,nikupongeze Mufti kwa uongozi mzuri.Tunafahamu ujenzi wa
msikiti mkubwa wa ghorofa tatu pale BAKWATA makao makuu unaendelea
.Katika ule msikiti ghorofa ya tatu kutakuwa na ofisi yako,chumba cha
kupumzika na chumba kikubwa cha kupokea wageni wako," amesema Makonda.
Ametumia
nafasi hiyo pia kumpongeza Raid Magufuli kutokana na uzalendo wake
kwaWatanzania ambapo kwa juhudi zake kuna miradi mkubwa ya maendeleo
unaendelea nchini kwetu."Tunakushukuru Rais kwa kazi mkubwa na nzuri
unayoifanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu."
No comments:
Post a Comment