A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, October 31, 2018

Serikali yaandaa Mpango Mkakati kupiga Msasa Wasaidizi wa Kisheria Nchini

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo Maalum ya Wawezeshaji watakaotoa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria ili waweze kupata usajiri rasmi na wa kisheria wa kutoa huduma za kisheria kwa wananchi. Mafunzo hayo yameandaliwa na Law School of Tanzania (LST) na kufadhiliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF) yaliofanyika Dodoma jana. (Mpiga Picha Wetu)

Serikali imeandaa mpango mkakati wa kutoa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria kama njia ya kuboresha huduma za msaada wa kisheria kwa watanzania maskini wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ya kisheria nchini.
Mpango wa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria nchini unatarajiwa kuanza mapema Mwezi Novemba, na walengwa wakuu ni wasaidizi wote wa kisheria ambao wanaotoa huduma za msaada wa kisheria katika maeneo mbalimbali nchi nzima.
Kama sehemu ya maandalizi ya mafunzo hayo, wiki iliyopita Serikali kupitia ofisi ya Msajili wa Watoa Huduma za Kisheria –Wizaraya Katika na Sheria, iliendesha mafunzo yaliyolenga kupika wataalum (wawezeshaji) wapatao 40 (kutoka mashirika mbalimbali ya huduma za kisheria) watakaoendesha mafunzo hayo maalamu kwa wasaidizi wa kisheria.
Mafunzo ya kupika wawezeshaji yalifanyika Dodoma, yaliandaliwa na Law School of Tanzania (LST) kwa kushirikiana na  Tanzania Law Society (TLS) na kufadhiliwa na shirika la  Legal Services Facility (LSF)—taasisi inayofadhiliwa miradi/shughuli  mbalimbali ya wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar.
Akiongea na gazeti hili jana, Mratibu wa Mafunzo ya Wawezeshaji, Bw.Suleiman Pingoni, amesema mafunzo hayo yanalenga kupika wataalam mahiri wakaoendesha mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria, yanayotajiriwa kuanza rasmi mapema Mwezi Novemba, na kumalizika kabla ya Disemba 31, Mwaka huu.
Mafunzo kwa wawezeshaji, kwa mujibu wa Bw.Pingoni, yalilenga kuwawezesha kupata ufahamu wa kutosha kuhusu maswala ya  msingi kuhusu sheria ya Msaada wa Sheria (Legal Aid Act ) ya Mwaka 2017 na Kanuni zake, matakwa ya sheria kuhusu usajiri na usaili wa wasaidizi wa kisheria. Sheria ya Msaada wa Kisheria inawataka wasaidizi wa kisheria kupata mafunzo maalum ili waweze kusajiliwa na kupewa leseni za kutoa huduma za kisheria kwa wahitaji.
“Kimsingi, sheria ya Msaada wa Kisheria imewatambua wasaidizi wa kisheria na kazi wanazofanya hivi sasa. Hata hiyo, sheria hiyo hiyo, inawataka wasaidizi hawa wa kisheria kupata mafunzo maalum ili waweze kupatiwa liseni/vitambulisho ili waruhusiwa kutoa  huduma za kisheria,” amesisitiza Bw. Pingoni.
Kwa mantiki hiyo, Office ya Msajili wa Watoa Huduma za Kisheria ameandaa mafunzo kwa wawezeshaji watakaotoa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria, ili waweze kukidhi matakwa ya sheria.
Mwisho wa siku, wasaidizi wa kisheria watakapata mafunzo hayo maalum watapatiwa vyeti, ambavyo vinawazesha kutuma maomba ya kusajiliwa na kutambuliwa kama wasaidizi wa kisheria kwa mujibu wa Sheria, na baada kupatiwa vitambulisho maalum, amesema Pingoni.
“Lengo kuu la michakato hii yote ni kupata wasaidizi wa kisheria mahiri na wenye uwezo, ambao wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, wakaoweza kutoa huduma bora na zenye viwango kwa wananchi, amesema Bw.Pingoni.
Akichangia, Mkurugenzi wa Mradi-LSF, Bibi. Scholastica Jullu ameelezea mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria kama “hatua kubwa katika jitiada za serikali na wadau wa huduma za kisheria zinazolenga kupanua wigo wa huduma za msaada wa kisheria na kuwezesha watu maskini, wanaodhulimiwa na kunyanyaswa kupigania na kupata haki zao.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages