A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, October 24, 2018

NBC yapongezwa kwa kudhamini maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji mjini Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila (wa pili kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa  Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo kutokana na udhamini wa benki hiyo katika maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji, programu na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonyesho hayo katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya jana. Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mariam Mtunguja.

Mkuu wa Uhai wa Wateja wa NBC Tanzania, Gaudence Shawa (kulia) akizungumza na Mshauri wa Kilimo na Huduma za Fedha Vijijini wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Samora Lupalla (katikati) huku Ofisa Habari wa mfuko huo, Victor Kyando akiangalia katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonyesho hayo katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya jana. Kushoto ni Meneja Mahusiano wa NBC Tanzania, William Kallaghe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wa pili kushoto), akipewa maelezo kuhusu huduma na bidhaa za kibenki zitolewa na Benki ya NBC na Mkuu  wa Kitengo  cha Uhai  wa Wateja wa benki hiyo,  Gaudence Shawa wakati wa maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji, programu na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na kumalizika  juzi katika  Viwanja vya Ruanda Nzovwe  Mkoani Mbeya
Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya, Jasmine Kilalile (kushoto), akitoa ufafanuzi wa faida za kujiunga na huduma mpya ya NBC Kikundi Mobile kwa baadhi ya wakazi wa Mbeya waliofika katika maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji, programu na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na kumalizika  juzi katika  Viwanja vya Ruanda Nzovwe  Mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages