A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, August 21, 2018

Wazazi watakiwa kuchangia chakula kukomesha utoro shuleni

simiyu1

Na Juma Mbonde
Halmashauri ya Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wametakiwa kuwakumbusha wazazi na walezi kuwanunulia watoto wao sare za shule na kuchangia chakula mashuleni ili watoto wao waweze kusoma kwa utulivu na umakini wanapokuwa shuleni  na  kuzuia utoro .

Rai hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru baina ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera yaliyofanyika katika Kijiji cha Mkula wilayani humo.

Kabeho amesema Serikali ya awamu ya tano imefuta ada na michango mbalimbali iliyokuwa kero kwa wananchi ili kila mtoto wa Kitanzania apate haki ya Elimu kuanzia darasa la awali mpaka Kidato cha nne bila malipo , hivyo wazazi na walezi wanapaswa kuwanunulia watoto wao sare za shule pamoja na mahitaji yao mengine ya shule ikiwa ni pamoja na daftari na kalamu.

“ Kwa sasa wazazi hamlipi tena ada wala michango  wajibu wenu ni kununua sare za shule na kununua mahitaji mengine kama kalamu, daftari na mabegi ,Serikali inaendelea kuhamasisha mtimize wajibu wenu, lakini pia namuomba Mkurugenzi awaeleze Walimu wakuu sare za Halmashauri yake ni zipi ili nao wawakumbushe wazazi kwanunulia watoto wao sare hizo” alisema.
Aidha, Kabeho amesema ni vema  wazazi  na walezi wakachangia chakula shuleni ili kuwafanya wanafunzi waweze kusoma kwa utuivu na umakini wanapokuwa shuleni  na  kuzuia utoro .

“Tunaomba pia mtimize wajibu wenu kuchangia chakula shuleni kwa sababu unapotoa chakula shuleni tunapunguza utoro , tunaongeza umakini na ufuatiliaji kwa wanafunzi pale wanapofundishwa, wanafunzi wengi wao wanatoroka pale wanapohisi njaa na wakiondoka baadhi yao hawarudi” alisema Kabeho.

simiyu2

Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Busega na kupitia miradi saba yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 900 katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu na Viwanda.

Akizungumza mara baada ya kufungua vyumba vitatu vya madarasa na matundu matano ya vyoo katika Shule ya Sekondari Nasa, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg.

Charles Kabeho ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ambayo itasaidia kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Akizungumza na Wananchi baada ya kufungua Wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Nasa Kabeho amewashukuru wananchi kwa namna wanavyojitolea nguvu kazi katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo katika Kituo hicho cha Afya cha Nasa.

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Wodi hiyo ya wazazi, Katibu wa Afya Wilaya wa Wilaya ya Busega Huruma Temu amesema kuwa wodi hiyo katika kituo cha Afya Nassa hadi kukamilika kwake imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 109 ikiwa ni fedha za wafadhili kutoka UNFPA.

Haruna alibainisha kuwa lengo kuu la kujenga wodi hiyo ya wazazi ni kuboresha afya ya uzazi na kupunguza idadi ya vifo vya akinamama na watoto Wilayani Busega

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages