Mgombea kiti cha Ubunge kwa tiketi ya CCM, Waitara jumapili hii alishiriki Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Huduma ya Neno la Upatanisho WRM linaloongozwa na Nabii Brother Nicolaus Suguye lililopo Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga, Dar es Salaam.
Mwita Waitara ni miongoni mwa Wabunge wawili waliojiunga na CCM hivi karibuni kutokea Vyama vya upinzani na sasa amechaguliwa na CCM kugombea tena Ubunge kwenye Jimbo hilohilo la UKONGA ambalo alikua Mbunge wake kupitia CHADEMA kabla ya kujiunga na CCM.

Wakati huu ambapo anajiandaa kuingia kwenye Uchaguzi wa marudio, Mwita amehudhuria ibada kwenye Kanisa la WRM Kivule Dar es salaam na kufanyiwa maombi na kiongozi wa Kanisa hilo Brother Nicolaus Suguye kama inavyoonekana kwenye picha.
Watu mbalimbali wamekua wakifika Kanisani WRM Kivule Matembele ya Pili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maombi wakiwemo Viongozi wa Serikali na wa Kisiasa ambapo mwingine ambae alikwenda hivi karibuni ni Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye.
Katika ibada hiyo Waitara alipata nafasi ya kuwasalimia waumini wa kanisa hilo na kuwaomba wamuweke kwenye maombi yao katika harakati zake za Siasa.
Nabii Brother Nicolaus Suguye, alipata nafasi ya kumuombea na kumuweka mikononi mwa Mungu, nakumpongeza Mhe. Waitara kwakufanya jambo jema kukimbilia nyumbani mwa Mungu kuhitaji msaada.
Pia Brother Suguye, alimpatia Mhe. Waitara vifaa vya Kiroho kwaajili ya Ulinzi wake, kazi yake na familia yake. Vifaa hivyo ni kama; Maji ya Ubavuni mwa Yesu, Mafuta ya Baraka na Uponyaji, Stika ya Ninalindwa na Uwe Hai Yesu Yu Hai, pamoja na Leso ambazo zimekuwa msaada mkubwa sana kwa waumini na watu mbalimbali wanazozitumia kutoka kanisani hapo.
Brother Nicolaus Suguye, akimpatia maelekezo Mhe. Waitara jinsi Stika ya Ninalindwa inavyofanyakazi na kuwasaidia watu mbalimbali wanayoitumia kama kifaa cha kiroho.
Brother Nicolaus Suguye, akimpatia Mhe. Waitara kofia ambayo alipatiwa kama zawadi kutoka kwa Kituo cha Televisheni kinachomilikiwa na Kanisa hilo cha WRM
Brother Nicolaus Suguye, akimpatia maelekezo Mhe. Waitara jinsi kutumia Maji ya Ubavuni Mwa Yesu na kumpa shuhuda mbalimbali jinsi yanavyofanyakazi na kuwasaidia watu mbalimbali wanayoitumia kama kifaa cha kiroho.
Brother Nicolaus Suguye, akimpatia maelekezo Mhe. Waitara jinsi kutumia Mafuta ya Baraka na Uponyaji na kumpa shuhuda mbalimbali jinsi yanavyofanyakazi na kuwasaidia watu mbalimbali wanayoitumia kama kifaa cha kiroho
Nabii Brother Nicolaus Suguye, alipata nafasi ya kumuombea na kumuweka mikononi mwa Mungu, nakumpongeza Mhe. Waitara kwakufanya jambo jema kukimbilia nyumbani mwa Mungu kuhitaji msaada.
Brother Nicolaus Suguye, akimpatia maelekezo Mhe. Waitara jinsi Stika ya Ninalindwa inavyofanyakazi na kuwasaidia watu mbalimbali wanayoitumia kama kifaa cha kiroho.
Brother Nicolaus Suguye, akimpatia Mhe. Waitara kofia ambayo alipatiwa kama zawadi kutoka kwa Kituo cha Televisheni kinachomilikiwa na Kanisa hilo cha WRM
Brother Nicolaus Suguye, akimpatia maelekezo Mhe. Waitara jinsi kutumia Maji ya Ubavuni Mwa Yesu na kumpa shuhuda mbalimbali jinsi yanavyofanyakazi na kuwasaidia watu mbalimbali wanayoitumia kama kifaa cha kiroho.
Brother Nicolaus Suguye, akimpatia maelekezo Mhe. Waitara jinsi kutumia Mafuta ya Baraka na Uponyaji na kumpa shuhuda mbalimbali jinsi yanavyofanyakazi na kuwasaidia watu mbalimbali wanayoitumia kama kifaa cha kiroho
No comments:
Post a Comment