Msanii wa filamu nchini Wastara Juma amedai anawachukia wanaume wenye
rangi nyeupe kwasababu wanakuwa na matatizo mengi pindi anapokuwa nao
katika mahusiano ya kimapenzi ndio maana kwa sasa anawapenda weusi kama
aliyokuwa nayo marehemu Sajuki.
Wastara amebainisha hayo wakati alipokuwa anajibu miongoni mwa maswali
yaliyokuwa yanaulizwa na mashabiki zake waliokuwa wanataka kufahamu ni
mwanaume wa aina gani Wastara anamvutia kuwa naye katika mahusiano ya
kimapenzi au kwa sasa endapo atatokea.
"Mimi kiukweli namtaka mwanaume ambae anajiamini ambae hata tukitembea
mbele za watu hawezi kuona aibu, anaejali, mwenye mapenzi ya dhati, awe
mwanaume wa kweli yaani asiwe 'Punga' ila asiwe na rangi nyeupe maana
nawachukia sana wenye rangi hiyo, nampenda mwenye rangi nyeusi", amesema
Wastara.
Aidha, Wastara amesema kipindi cha awali alipokuwa anaanza kujihusisha
katika masuala ya mapenzi alikuwa na vigezo vingi alivyokuwa anavitaka
awe navyo mwanaume kama kifua kikubwa, Six Pack na vinginevyo.
"Kwa sasa sitaki vigezo kwasababu nimejifunza mengi kutoka kwa marehemu
Sajuki maana mume wangu alikuwa na Six Packs za ukweli lakini alipokuwa
anaumwa zote zikaondoka 'so' kutoka hapo nimejifunza kupenda jinsi
mwanaume alivyo maana vingine vinakuja na kuondoka wakati wote",
amesisitiza Wastara.
Kwa upande mwingine, Wastara amesema yupo tayari hata sasa kuolewa na
mwanaume mwingine ambaye wataridhiana wenyewe kwa kuwa dini yake ya
kiislamu inampa fursa ya kuolewa mpaka pale kifo chake kitakapomchukua
endapo hatakuwa katika ndoa.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, March 15, 2018
Wastara afunguka kuwachukia wanaume wenye rangi nyeupe
Tags
FILAMU#
Share This
About kilole mzee
FILAMU
Labels:
FILAMU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment