Kikosi cha Simba kikiwa kimeondoka nchini kuelekea Masry kwa ajili ya
mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry,
kocha wa Mbao Etienne Ndayiragije amesema kila kitu kinawezekana kwenye
soka na Simba inaweza kupata matokeo ikiwa ugenini.
Simba itacheza mechi ya marudiano dhidi ya Al Masry ugenini baada ya
kutoka sare ya kufungana 2-2 kwenye mechi ya awali iliochezwa uwanja wa
taifa.
“Kilakitu kinawezekana kwenye football, walicheza dakika 90 nyumbani
wanakwenda kucheza nyingine ugenini, uwanja ni uleule pitch ni ileile ni
jinsi gani wamejipanga Mungu akiwajalia kila kitu kinawezekana.”
“Wanatakiwa kujua hii siyo ligi ni mechi za mtoano, ukiwa ugenini kama
unajiaandaa na hizi mechi za Caf unatakiwa kushambulia kwa sababu hauna
haja ya kujilinda. Nikiangalia aina ya wachezaji ambao Simba inao
wanauzoefu wa kufunga wakipata nafasi watafunga.”
“Wakijiandaa kwa ajili ya kujilinda sijui itakuwaje itategemea na namna ambavyo mwalimu ame-plan.”
Kocha huyo amesema, kiufundi mechi za aina hiyo zinategemea mambo mengi
sana nje na ndani ya uwanja ambayo yanaweza kuleta ushindi au kinyume
chake.
“Mechi kama hizi zinatemea na jinsi mtakavyosafiri, watafika lini,
watafikia wapi, hali ya hewa ilivyo, nayo huwa inachangia kwa asilimia
kubwa.”
Kama unakumbuka Mbao ikiwa chini ya Etiene ilicheza na Simba fainali ya
FA Cup na kupoteza mchezo huo kwa mufungwa 2-1 Simba wakabeba ndoo
iliyowapa tiketi ya mucheza Caf Confederation Cup, endapo Mbao
wangeshinda mechi hiyo wangekuwa wawakilishi wa nchi katika michuano ya
Afrika.
Etiene amesema endapo Mbao ingekuwa inashiriki mashindano ya kimataifa
anadhani ingepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau nchini hivyo
wangesajili na kufanya maandalizi ya kutosha, uzoefu wake kwenye
mashindano ya kimataifa ungeisaidia timu.
“Kwanza ikitokea umepata nafasi ya kushiriki matokeo yanatokana na
maandalizi. Ingekuwa ni Mbao ndio inawakilisha Tanzania naimani kuwa
uongozi wa timu, mkoa hadi nchi ungesapoti sana maandalizi si dhani kama
kina Buswita na wengine wangeondoka kwenye klabu.”
“Wangepatikana wadhamini tungesajili na kujiandaa na maandalizi
yasingekuwa kama ilivyo sasa hivi. Najua kwa sababu nimeshashiriki kombe
la shirikisho nikiwa kocha Vital ‘O na Ngaya Club najua nini
kinahitajika kwa hiyo ningejiandaa. Zote nilizifikisha mechi za mwisho
kabla ya makundi.”
Kuhusu mapungufu aliyoyaona kwa Al Masry ambayo Simba wanaweza kuyatumia
ikawa faida kwao, kocha huyo amesema kila timu ina mapungufu na uwezo
wake lakini pia inategemea plan za kocha kwa mchezo husika.
“Katika mpira kila timu inakuwa na mapungufu yake lakini inakuwa na
uwezo wake pia, hizi ni mechi ambazo unatakiwa kucheza kitimu (mwalimu
ndio anatoa plan ya mechi). Kutokana na mechi anajua atalinda wapi,
niwasubiri katikati, niwafuate kwao au niwasubiri kwetu hayo ni maamuzi
ya kocha kulingana na alivyouona mchezo.”
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, March 15, 2018
Kocha wa Mbao asema Simba inaweza kupata matokeo ikiwa ugenini
Tags
MICHEZO#
Share This
About kilole mzee
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment