Ubalozi
wa Tanzania nchini Ufaransa ambao pia unawakilisha Tanzania katika nchi
ya Hispania kwa kushirikiana na Shirikisho la wafanyabiashara la Madrid
(Madrid chamber of commerce – CAMARA) pamoja na Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC) uliandaa kongamano la kwanza la biashara na uwekezaji
kati ya Tanzania na Hispania tarehe 12/03/2018 mjini Madrid.
Kongamano
hilo liliudhuriwa na watendaji wakuu wa makampuni makubwa Madrid nchini
Hispania yapatayo 60. Kongamano hilo lilifunguliwa na Bw. Augusto de
Castaneda, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara la Madrid.
Katika kongamano hilo, Mhe. Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini
Hispania, mwenye makazi nchini Ufaransa, aliyashawishi makampuni hayo
kuja kuwekeza nchini Tanzania.
Balozi
Shelukindo alieleza juhudi mbalimbali alizozichukua Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamuhri ya muumngano wa Tanzania katika
kupambana na rushwa jambo ambalo limetengeza mazingira bora ya kufanya
biashara na kuwekeza nchini. Balozi Shelukindo alieleza kwamba hali ya
utulivu na usalama ambayo imeendelea kuwepo nchini Tanzania imekuwa ni
kivutio kikubwa cha uwekezaji kutoka nje.
Bw.
Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) ambaye alishiriki katika kongamano hilo aliezea mazingira bora ya
uwekezaji nchini pamoja na fursa mbalimbali zinazoweza kupatikana
Tanzania.
Pia
aliendelea kuelezea jinsi Kituo cha Uwekezaji kilivyojiandaa kuwapokea
wawekezaji kutoka Hispania kuja kuwekeza nchini kwa kuwasaidia kujua
taratibu na sheria mbalimbali zinazohusu uwekezaji nchini. Aidha Bw.
Mwambe alielezea fursa za kipaumbele ambazo ni viwanda, kilimo,
miundombinu pamoja na nisharti.
Bi.
Devota Mdachi, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) alitoa
mada kuhusu vivutio vya utalii vinavyopatikana nchini Tanzania na
kuyakaribisha makampuni ya Hispania kuja kuwekeza katika sekta hiyo
muhimu katika uchumi wa Tanzania.
Bw.
Gilead Teri Mkurugenzi wa Sera kutoka Taasisi ya sekta binafsi Tanzania
(TPSF) alielezea mchango wa sekta binafsi katika uchumi wa Tanzania na
namna Taasisi hiyo itakavyoshirikiana na wawekezaji kutoka Hispania.
Baada
ya kongamano hilo Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara la
Madrid Bw. Augusto de Castaneda aliahidi kwamba wafanyabiashara na
wawekezaji kutoka Hispania watafanya ziara nchini Tanzania hivi karibuni
kuchangamkia fursa hizo.
Mheshimiwa,
Samwel Shelukindo Balozi wa Tanzania nchini Hispania mwenye makazi
Ufaransa , Makamu wa Rais wa Madrid Chamber of Commerce Bw. Augusto de
Castaneda Bw. Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania na Bi. Devota Mdachi, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB) wakiwa kwenye meza kuu wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wawakilishi wa makampuni ya Kihiispania walioshiriki kwenye kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment